in

Programu Mpya za Android Ambazo ni Bora Kuwa Nazo Mwezi Huu

Programu mpya za Android za kuwa nazo mwezi huu wa Nane

Kila siku programu mpya za android huwekwa kwenye soko la Play Store na hii husababisha watu wengi kushindwa kujua programu bora ambazo zinaweza kukusaidia pale unapokuwa na simu yako. Ndio maana leo tunakuletea list hii ya programu mpya za android ambazo ni nzuri kuwa nazo..

Holo – Holograms for Videos in Augmented Reality

Holo ni app nzuri na bora sana kuwa nayo app hii inakusaidia kuleta uwezo tofauti wa picha na video kwenye simu yako, app hii inaweka uwezo mpya kwenye kamera yako kwa kuongeza vitu mbalimbali pale unapo piga picha.. angalia video hapo chini. kisha download app hii utaipenda.

Control Center IOS 11

Control Center iOS 14

Kama umekua kwa muda ukitamani muonekano wa simu za iPhone basi hii ni habari njema kwako kwani app hii itakusaidia kuweza kupata sehemu ya mfumo wa iPhone, sehemu hii ni ile ambayo imetoka hivi karibuni inayoitwa Control Center sehemu hii itakusaidia kufanya vitu haraka haraka na kwa urahisi kabisa bila kuingia kwenye setting za simu yako..

Face Swap

Face Swap
Price: Free

Hii ni programu nyingine bora kutoka kwa kampuni ya microsoft programu hii itakupa uwezo wa kubadilisha sura yako na kuiweka kwenye baadhi ya picha zingine. Uzuri wa app hii ni kuwa inauwezo mkubwa sana wa kubadilisha picha yako ijaribu sasa uone..

Badilisha Muonekano wa Simu Yako kwa Wallpaper Hizi

BatON

BatON
Price: Free

Hii ni programu bora sana kwa wale wanaotumia vitu vyenye kutumia wireless na bluetooth. Programu hii itakusaidia kuweza kujua kiasi cha battery kilicho baki kwenye vifaa vyako vya bluetooth kupitia kwenye simu yako. unachotakiwa ni kutafuta kifaa chako kupitia programu hii kisha itakwambia ni kiasi gani cha chaji kilicho baki kwenye kifaa chako kupitia simu yako, ijaribu sasa uone.

Teleport – photo editor

Hii ni programu nyingine bora kwaajili ya picha na ubora wake upo kwenye uwezo wake wa muonekano wa picha yako kwa nyuma yani background image programu inauwezo mkubwa sana wa kubadili picha hivyo kama unapenda kubadili picha na kucheza na filter programu hii ni bora kwako ijaribu sasa.

Skippy: YouTube turned into books

Hii ni programu bora sana kwa watumiaji wa mtandao wa Youtube, programu hii itakusaidia kusogeza mbele video mpaka kwenye sehemu zile za muhimu. Yaani programu hii inajua kabisa ni sehemu gani za muhimu wewe kuangalia kwenye video ndevu hivyo kwa kusogeza mbele inakuwa ikiondoa zile sehemu ambazo hazina maana na kuacha video kuwa fupi na yenye maana kwako.

Njia 4 Bora za Kusaidia Kukumbuka Password Yoyote (2020)

Na hizo ndio programu mpya nbilizo kuandalia leo ambazo kwa namna moja ama nyingine zinauwezo wa kubadilisha matumizinya simu yako ya android kuwa bora zaidi na rahisi lakini kabla ya kumalizia…one more..!

Tanzania Tech

Kama bado uja download app ya Tanzania Tech basi unapitwa na mengi kwani app hii itakupa uwezo wa kupata habari zote za teknolojia kwa haraka na kwa kupitia simu yako ya mkononi ya Android, kama unataka habari za teknolojia kila siku basi nakushauri kudownload app hii sasa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 4

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.