Sasa Chukua Picha za Nyuzi 360 Kwenye App ya Facebook

Sasa tumia picha mbadala za nyuzi 360 kupitia App ya Facebook

Kwa wapenzi wa mtandao wa kijamii wa Facebook mambo yanaendelea kuwa mazuri kwani sasa unaweza kuchukua picha za nyuzi 360 moja kwa moja kupitia app yako ya Facebook ya Android pamoja na iOS.

Mwanzoni kabla ya sehemu hii kuletwa ndani ya App za facebook ilikuwa inakubidi kutumia app za pembeni ili kuweza kuchukua picha za nyuzi 360 na ndipo baadae uiweke kwenye uwanja wako wa akaunti ya facebook.

Hata hivyo kwa hapa Tanzania naona matumizi hayo hayakuwa makubwa sana au hayakuwa yakijulikana lakini sasa unaweza kufanya hivyo moja kwa moja kupitia app yako ya Facebook, unaweza kujaribu sasa hivi..

Uzuri ni kwamba unaweza kuweka picha ya nyuzi 360 kwenye profile yako hivyo watu wanaweza kuona zaidi ya picha kupitia App yako ya Facebook.

Kama bado hujajua jinsi ya kutumia sehemu hiyo basi hivi ndivyo unavyofanya. Ingia kwenye app yako kisha fanya kama unataka kuandika kitu kwenye ile sehemu ya Status, kisha utaona menu nyingi zikitokea chagua sehemu ya mwisho imeandikwa 360 Photo kisha fuatisha maelezo utaweza kuchukua picha yako ya nyuzi 360.

Apps Nzuri za Kusaidia Ku-forward Meseji Kwenye Simu Yako

Unaweza kutuma picha hiyo kwenye uwanja wako wa Facebook kawaida au unaweza kuweka picha hiyo kwenye sehemu yako ya cover picture, nadhani hii ni sehemu nzuri sana inayoweza kuleta picha zenye kuonyesha mambo mengi zaidi ya upande mmoja tu… ijarubu sehemu hii sasa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : TechCrunch

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.