Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph nchini Tanzania, Coreen Swai amefikia hatua nzuri ya masomo yake kwa kutumia elimu aliyoipata chuoni hapo kuweza kufanya ubunifu wa fimbo ya kidijitali au “Smart Blind Stick” kama alivyo ipa jina mwenyewe.
Coreen ameweza kufanya ugunduzi huo baada ya kuamua kufikiria namna ya kipekee ya kuwa saidia walemavu wa macho hasa pale wanapotaka kutembea safari za umbali mrefu.
Coreen ambae anasoma kozi ya Information Systems and Networking Engineering anatarajia ugunduzi huo utawasaidia walemavu wengi wa macho hasa kutokana na uwezo wa fimbo hiyo wa kutoa mlio maalum pale mlemavu wa macho anapo kutana na kitu mbele yake.
Ugunduzi huu ni moja kati ya gunduzi bora mbalimbali ambazo zimewahi kufanywa na watanzania hivyo nadhani ni wakati sasa serikali kupitia Costech na wizara husika kuona vipaji vya watanzania hasa kwenye ulimwengu huu wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Vdeo.
Chanzo : DW Swahili