Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mkuu wa Kampuni ya Samsung Lee Jae-yong Ahukumiwa

Mrithi wa kampuni ya Samsung sasa kuhukumiwa miaka mitano
Samsung Lee Jae-yong Samsung Lee Jae-yong

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya BBC Swahili, Mahakama nchini Korea Kusini imemhukumu bilionea anayetarajiwa kurithi kampuni ya Samsung Lee Jae-yong kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya utoaji rushwa.

Bw Lee alikuwa ameshtakiwa kuhusika katika rushwa katika kashfa ambayo pia ilichangia kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Korea Kusini Bi Park. Kesi hiyo ilikuwa imevutia sana umma huku hasira zikiendelea kupanda dhidi ya makampuni makubwa ya kibiashara ya Korea Kaskazini, maarufu kama chaebols.

Advertisement

Bw Lee, ambaye amekanusha mashtaka yote, alikuwa amekabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela hadi miaka 12, lakini hatimaye mahakama imeamua kumhukumu leo miaka mitano. Hata hivyo Miongoni mwa makosa aliyokabiliwa nayo ni utoaji rushwa, wizi wa mali ya umma pamoja na kuficha mali nje ya nchi.

Lee, mwenye miaka 49, pia alituhumiwa kutoa mchango wa hisani wa won 41bn ($36m; £29m) kwa nyakfu za hisani zilizosimamiwa na rafiki wa karibu wa rais aliyeondolewa madarakani Park Geun-hye.

Bw Lee, ambaye pia hufahamika kama Jay Y Lee na amekuwa ndiye kiongozi wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuunda simu duniani na amekuwa kizuizini tangu Februari akikabiliwa na tuhuma kadha za rushwa.

Hukumu hiyo imetilia shaka sasa uongozi wa Lee katika kampuni ya Samsung, kwani amekuwa kaimu mwenyekiti tangu babake Lee Kun-hee alipopatwa na mshtuko wa moyo mwaka 2014.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : The Verge

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use