Kampuni kubwa zaidi ya mitandao ya kijamii duniani Facebook, inatarajia kuanza kutoa huduma ya video itakayokuwa ikiitwa ”watch” ama tazama, sehemu hiyo imebuniwa ili kushindana na televisheni za kawaida pamoja na mitandao ya Video kama vile Youtube, Netflix, Twitter pamoja na snapchat.
Sehemu hiyo itakuja kwa mfumo wa Tab au ukurasa maalaum ndani ya Facebook ambapo hapo utaweza kuangalia video ambazo zitakuwa kwa mfululizo au mtiririko maalum (episodes).
Sehemu hii tayari imesha anza kufanya kazi kama hatua ya majaribio nchini marekani, ina tarajiwa kuanza kufanya kazi nchini humo mapema mwezi huu na baadae kusambaa nchi zingine duniani kote, hata hivyo Facebook tayari ina vipindi kadha vikiwemo vya michezo, vya familia na vya televisheni ya National Geographic tayari kuanza kuonyesha kwenye sehemu hiyo.
Facebook inasema kuwa imewekeza mamilioni ya dola katika kuifanya huduma hiyo kupendwa zaidi na kutumiwa zaidi na watumiaji wa mtandao wa facebook na wengine kutoka kwenye mitandao mingine.
Kwa sasa mitandao ya kijamii inaonekana kuwekeza sana kwenye upande wa video kwani hivi karibuni Instagram inategemewa kufanya maboresho ya Live Video, huku youtube nayo hapo jana imeongeza sehemu mpya ya share kwenye app zake za Android na iOS. Bado tunasubiri kwa upande wa WhatsApp kujua itakuja na nini..
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : Facebook Newsroom