Mamlaka ya Maji Jijini Dar es Salaam Yaja na DAWASCO App

Mamlaka ya maji jijini Dar es Salaam yaja na App Yake
DAWASCO DAWASCO

Mamlaka ya maji safi na taka jijini Dar es salaam, leo imetangaza kuja na programu yake mpya ya Android kwaajili ya kusaidia wateja wake wa jijini dar es salaam kwa urahisi zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia ‘TEHAMA’ wa DAWASCO’, Kiula Kingu amesema kuwa lengo kuu la mfumo huu ni kumweka mteja karibu kihuduma.

Hata hivyo akielezea jinsi app hiyo inavyofanya kazi, amesema kuwa mteja wa dawasko au hata ambaye si mteja ataweza kutoa ripoti mbalimbali za kupasuka kwa bomba ili kurahisha wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuzuia matatizo hayo.

Advertisement

App hii kwa sasa inapatika kupitia Play Store na unaweza ku-download app hiyo kwa kubofya link hapo chini, App hii ni bora sana kwani inafanya vitu vingi kwa wakati mmoja na inakupa taarifa zako papo hapo.. ijaribu sasa bofya hapo chini kudownload.

DAWASA
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Millard Ayo

1 comments
  1. Ndugu Dawasco,
    Nafurahi sana kwa mpango mzima mlioubuni kwa kumtua mama ndoo kichwani ya Maji.Hii inadhihirisha mnapiga hatua ndefu kumfikia kila mmojawetu kupata huduma hii muhimu sana ukilinganisha na mahitaji mengine,Sio kwamba hakuna mahitaji muhimu kama maji, la Hasha , bali ni kutokana na uhalisia wenyewe jinsi ulivyo.
    Mmeweza kuboresha maeneo mengi ya maji, hususani vijijini na mijini, na katika zoezi, hilo hapakosekani changamoto zitakazo jitokeza, Kila jambo zuri linalofanyika, kuna mitihani yake,Kweli katika wizara, , sekta, na idara zote zinazo husika na mfumo huu wa utekelezaji wa kuboresha maji pembe zote za miji na vijiji, tunaungana na nyie wote kwa jukumu hili zito na na la muhimu kwa jamii kutoteseka kwa ukosefu wa maji.
    Sasa nije kwenye maoni yangu,Kwanza kwa majina ni Dennis E.Munuo, naishi mbezi msakuzi,na kumbuka tangu 2007 nilipo hamia huko, hadi napoandika nakala hii, eneo kubwa la mpige na kwingineko maji ni ALMASI.Mimi katika eneo letu la msakuzi kata ya kwembe, tulijichangisha fedha takribani wapatao zaidi watu 60, kila kaya kutoa shs laki nne(400,000/=taslimu,kwa kuomba majirani zetu wa MSHIKAMANO, BARABARA YA KONIKE,ambao walibahatika kuvuta maji kwa nguvu zao, tuunganishe mpira wetu, hakika zoezi lilifanyika na mwishowe tukawahusisha wana dawsco, ili kuwaonyesha kiu yetu na juhudi zetu zimefikia wapi, kweli walitupongeza, na kuweza kuungana nasi kwa zoezi la kutuwekea mita za maji pamoja na mambo ya finishing, tukashukuru Mungu hata kwa zoezi hilo, Nakumbuka kwa mara ya kwanza maji kutoka ilikuwa ndani ya wiki hiyo tu baada ya zoezi kumalizika, nadhani sijui kwa nyumba zingine, watoto walishangilia na kurukaruka kwa kuona maji yanatoka kwenye bomba la nyumbani, hakika kila baada ya siku zilivyokuwa zinapita ndivyo ugumu wa maji yalivyokuwa ngumu kutoka, hatimaye kwa kipindi cha miezi sita sasa maji ni hadithi, hivyo tumerudi katika zoezi la kudumu la kunua maji kama nyakati zote, kweli kununua maji ya kwenye gari, inaumiza sana, haswa wenye kipato kidogo cha kujikimu,Mimi naona kuna mkono wa mtu, haswa kwenye hii biashara ya maji,kwa uwelewa wangu wenye magari wemejiwekia ndipo biashara kwao ambayo haina usumbufu, hivyo kweli tunaumia sana, kama kweli mnataka jamii na vizazi vifaidike kwa kufurahia matunda toka wizara hii muhimu ya maji, basi muwe na mkono mrefu kufatilia udhalimu unaotendeka juu ya wananchi wa mpigi magoe.

    Narudia tena kuwapongeza kwa judhudi mlionao kwa kuboresha miundo mbinu ya maji. Napatikana kwa simu namba 0719 842675, Mungu awape wepesi katka ujenzi wa Taifa.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use