Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Dalili za Ugonjwa wa Kupenda Smartphone Kupita Kiasi

Ni vyema kujua kama una tatizo la kupenda simu kupita kiasi
kupenda simu kupita kiasi kupenda simu kupita kiasi

Ukweli ni kuwa wengi wetu tunapenda simu zetu, pengine hii ni sababu ya simu hizi kutupa uwezo wa kufanya mambo kwa urahisi na haraka sana lakini kila jambo likizidi basi kwa namna moja ama nyingine lina weza kuwa sumu kwenye maisha yetu ya kila siku. Hivyo basi kaa tayari kujua kama wewe una tatizo au (ugonjwa) wa kupenda simu kupita kiasi.

Kwanza napenda niseme kuwa kupenda simu yako kupita kiasi ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine ya tabia ya kupenda vitu kupita kiasi yaani (addiction), magonjwa haya hu-tibiwa kwa kupewa mazoezi ya kila siku ya ubongo ili kuweza kuacha tabia hizo.

Advertisement

Kwa mujibu wa tovuti ya addiction tips kama huto tibu ugonjwa wa kupenda simu kupita kiasi unaweza kupata matatizo mbalimbali ya afya kama vile, matatizo ya ubongo pamoja na kansa hivyo ni vyema kuanza kuacha tabia hii kama utajigundua unazo dalili zifuatazo.

  • Unashika Simu Yako Mkononi Muda Mwingi

Mara nyingi watu wenye tatizo la kupenda simu kupita kiasi hawawezi kukaa mbali na simu zao, mara nyingi hushika simu zao mkononi au kuziweka karibu nao au wakati mwingine utawakuta wanatumia programu tofauti kwenye simu au kuchati. Mara nyingi watu hawa hawawezi kukaa mbali na simu zao na ikitokea wako mbali na simu zao hushtuka na kuwa na hisia simu imepotea.

  • Lazima Uwe na Simu Yako Kila Siku

Inaeleweka kuwa na simu yako kila siku ni kitu cha muhimu tena ukizingatia kwenye ulimwengu wa sasa, lakini kama unajikuta kwenye wakati kuwa umesahau simu yako au umepoteza basi unakosa raha kabisa hata kama ulikua unauwezo wa kubadili line na kuendelea na mawasiliano basi jua kabisa inawezekana una tatizo la kupenda simu kupita kiasi.

  • Unakuwa na Wasiwasi wa Kupoteza au Kuibiwa Simu

Kuwa na wasi wasi wa kuibiwa au kupoteza kitu huwa ndani yetu sote lakini ni tatizo pale mtu anapokua ana wasiwasi kupita kiasi, hivyo kama umekua natabia hii kwa muda mrefu sasa ni vyema kuanza kujifunza kuacha kwani inawezekana una tatizo la kupenda simu kupita kiasi.

  • Unaingia na Simu Yako Chooni

Kama unayo tabia ya kwenda na simu yako kila mahali mpaka chooni basi ukweli ni kwamba lazima utakuwa na tatizo la kupenda simu kupita kiasi. Vilevile zaidi ya hayo unaweza kupata matatizo mengine ya kiafya kwa kwenda na simu chooni.

  • Unatumia Mitandao ya Kijamii Masaa 24

Mitandao ya kijamii ime tengenezwa ili kufurahia na kuunganisha watu lakini kuna wakati mwingine unakuta mtu yupo kwenye mitandao hiyo masaa yote na hapati hata muda wa kufanya mambo mengine na kama atakuwa anafanya mambo mengine lazima atakuwa na uwezo wa kuchati kupitia mitandao hiyo, kama unayo hii tabia kuwa muangalifu inawezeka una tatizo la kupenda mitandao ya kijamii kupita kiasi tatizo ambalo hupelekea kupenda simu kupita kiasi.

  • Unangalia Simu Yako Kila Saa, Mara Nyingine Bila Sababu

Kuangalia simu ni jambo la kawaida lakini kama unajikuta unatabia ya kuangalia simu yako kilamara hata kama huna jambo lolote la msingi unalo fanya basi, moja kwa moja unaweza kuanza kutambua kuwa unalo tatizo la kupenda simu kupita kiasi.

  • Unashika Simu Yako Mara tu Unapo Amka na Mara Unapo Lala

Hapa naomba tuelewane kwani si maanishi kushika simu pale unapokua na ratiba nyingine usiku hapana, hapa na maanisha pale unapokua kitandani unapo tafuta usingizi nilazima ushike simu yako au pale unapo amka asubuhi hata kabla ya chochote unashika simu yako kwanza. Kama una dalili hii kwa muda sasa ni vyema uka fikiria kuiacha kwani inawezekana una tatizo la kupenda simu hupita kiasi.

  • Unahisi Simu Yako Inaita Hata Kama Haiti

Kama umefikia hatua unahisi kama simu yako inaita na wakati haiti basi jua kuwa inawezekana unalo tatizo hili na mbaya zaidi ni pale unapo fikia hatua ya kuhisi hivyo mara zaidi ya moja kwa siku na mara nyingi zaidi kwa wiki.

  • Ukitembea Unashika Simu Mkononi Badala ya Kuweka Mfukoni

Mara nyingi tukiwa kwenye mwendo hatuwezi kutumia vizuri simu zetu, lakini kama unaona mara nyingi unatatizo la kushika simu yako mkononi huku ukitembea hata kama huitumi basi kuna uwezekano una tatizo la kupenda simu kupitiliza.

  • Unakimbilia Kushika Simu Yako Unapopata Tukio la Aibu

Kupata aibu ni sehemu ya maisha ya kawaida lakini kama unajikuta kwa mara nyingi pale unapo pata aibu flani unakimbilia kushika simu yako basi jua kabisa uwezekano upo kuwa una tatizo la kupenda simu kupita kiasi.

  • Unatumia Simu Yako Hata Unapo Kuwa Unangalia TV

Hii sio sawa na mtu kuwa amechoshwa na kitu flani ukiwa mahali fulani, bali hii ni pale unapokuwa nyumbani unakuta unao uwezo wa kuzima au kubadilisha channel kwenye TV yako lakini unajikuta unatumia simu yako huku unangalia TV. Kama kwa namna yoyote unayo tabia hii uwezekano wa kupenda simu kupita kiasi ni mkubwa.

  • Unakuwa Unafanya Kazi za Muhimu Kupitia Simu 

Hapa nazungumzia, kwa mfano mara nyingi unajikuta unajisikia vizuri kutuma barua pepe kwenye simu zaidi ya kutumia kompyuta hata kama unayo na hata kama barua pepe hiyo ni ndefu na inahitaji umakini. Kama unatabia hii ni vyema kuwa mwangalifu.

  • Muda Unaenda Sana Ukitumia Simu Yako

Hapa na maana kuwa mara nyingi unajikuta unatumia simu yako mpaka unashtuka hivi kumbe muda flani umefika..!, kama unayo tabia hii na imetokea mara nyingi sana basi unalo tatizo hili.

  • Simu Kwako ni Kitu cha Muhimu Kuliko Kitu Chochote

Kama unayo tabia ya kujali simu yako kuliko kitu chochote kile basi inawezekana kabisa unalo tatizo hili la kupenda simu kupita kiasi.

Na hizo ndio baadhi tu ya dalili ambazo leo nimeweza kukuchambulia ili kuweza kujua kuwa una tatizo la kupenda simu kupita kiasi, Tatizo hili linaweza kuisha kwa kujizoesha mambo mbalimbali kama kucheza mpira mazoezi au vitu vingine kama hivyo.

Ni vyema uka amua kumuona mshauri kama utashindwa kabisa kuacha tabia hii kwani, hili ni tatizo sugu kama yalivyo matatizo mengine ambayo ni ngumu kuyaAcha, kumbuka kupenda simu kupita kiasi kunaweza kusababishia matatizo mbalimbali kama ya Afya, matatizo ya kifamilia, kimahusiano na mambo mengine kama hayo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Addiction Tips

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use