Je Wajua Baadhi ya Battery za Simu Zinatuhumiwa Kuwa na Sumu

Kuwa muangalifu na aina ya battery inayotumiaka kwenye simu yako
battery battery

Zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya imeripoti BBC.

Utafiti huo ulibaini gesi 100 zenye sumu zinazotolewa na betri za Lithium, ikiwemo ile ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira.

Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.

Advertisement

Katika utafiti huo mpya, walichunguza betri moja ya kuchaji inayo julikana kama Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka. ”Siku hizi, Betri za Lithium-ion hukuzwa na serikali nyingi duniani kama kawi inayo patikana kwa haraka ili kuviwasha vifaa vyote ikiwemo magari ya kielektroniki hadi simu,” alisema Jie Sun, profesa mkuu katika taasisi ya ulinzi ya NBC.

Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa ikiwemo Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.

Hivyo ni vizuri kusoma maelezo ya aina ya battery kifaa chako inachotumia na ni vyema kukaa mbali na vifaa viavyo pata joto la battery lisilo la kawaida, pia kumbuka simu kupata moto sio kitu kizuri na inaweza ikawa ni dalili ya mambo mbalimbali kwenye simu yako kujua zaidi soma hapa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : BBC Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use