in

Wanasayansi Sasa Kutumia Wi-Fi Kujua Unavyojisikia Mwilini

Pia huweza kutumia teknolojia hii kujua mawazo yako

Wanasayansi kwenye chuo cha sayansi na teknolojia cha huko marekani MIT (Massachusetts Institute of Technology) wamefanikiwa kugundua aina mpya ya teknolojia ya kuweza kujua binadamu anavyojisikia, Wanasayansi hao wameweza hatua hiyo kwa kutumia mchanganyiko wa teknolojia za AI (Artificial intelligence) pamoja na Wi-Fi ili kuweza kutambua hali ya mwili wa binadamu.

Hata hivyo wanasayansi hao wame-tengeneza kifaa ambacho kinakuwa kwenye mfumo wa kifaa cha kawaida cha internet maarufu kama (router) au kifaa kinacho wezesha internet ya masafa marefu ndani ya nyumba au ofisi yako ambapo unaweza kuendelea kutumia internet ya Wi-Fi inayotokana na kifaa hicho huku chenyewe pia kina-endelea kusikiliza hali ya mwili wako.

Kifaa hicho (Router) hutumia miale ya RF signals ambayo hutolewa na kifaa hicho ili kusikiliza mapigo ya moyo wako ili kutambua hali ya mwili wako, hata hivyo kifaa hicho kinafanya kazi sawa na kifaa kinachotumia kwenye ma-hospital ili kujua mapigo ya moyo ya mtu pale anapokua amezidiwa kwa kitaalamu kinaitwa EKG au ECG. Lakini utofauti unakuwa kifaa hicho cha MIT hakitaji kufungwa kwenye mwili wa mtu kama kifaa cha EKG ili kutambua mapigo ya moyo wako bali chenyewe huwa mbali kabisa na wewe lakini huweza kusikiliza mapigo ya moyo wa binadamu kwa kutumia miale hiyo ya RF Signals.

Sunday Movie #4 : Movie Nzuri ya Teknolojia Kuangalia Jumapili

Hata hivyo hakijaishia hapo kwani wataalamu hao wanasema kifaa hicho kina uwezo wa zaidi wa kuweza kugundua mawazo ya binadamu kwa kusikiliza mapigo ya moyo wako tu.., watalamu hao wanasema kuwa kifaa hicho kinatumia teknolojia ya kisasa ya AI au (Artificial intelligence) kuweza kutafsiri mapigo ya moyo wako ili kuweza kufanikisha hatua hiyo ya kujua unacho kiwaza kwa wakati huo.

Kwa sasa waandishi maarufu kutoka kwenye tovuti mbalimbali maarufu nchini marekani wamekua wakihoji ujio wa teknolojia kama hizi kwani hata watu wabaya wanaweza kuzitumia kufanya uhalifu na mambo mengine kama hayo, huku ukizingatia teknolojia kama hii kutoka MIT ambayo mtu kuweza kujua unachowaza pamoja na hali ya mwili wako hata pale anapokua hatua chache tu kutoka ulipo..Mhh!

Lakin yote ya yote, kifupi ni kuwa teknolojia inaendelea kukuwa kila siku tupende au tusipenda na kutokana na sisi wote kujua kuwa chochote kizuri kinaweza kutumiwa kwa ubaya basi ni vyema kujiweka tayari na kujifunza teknolojia kwa haraka kwani tuwe tayari au tusiwe huko ndipo tunapo elekea… Hebu tuambie nini maoni yako kuhusiana na hili.? teknolojia kama hizi zinaweza kuokoa maisha lakini pia zinaweza kuhatarisha maisha ya binadamu, tuambie mawazo yako hapo chini.

App Nzuri Soko Maalum Kwaajili ya Kutambua Application Nzuri

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : The Next Web

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.