in

Video 10 Zinazoingiza Pesa Nyingi Kupitia Mtandao wa Youtube

Kama ulikua hujui wingi wa views kwenye video yako ndio kiasi cha pesa

Youtube ni moja kati ya mtandao maarufu sana na umarufu wake umefanya mtandao huo uwe ni sehemu ya kujitengenezea kipato kwa watu mbalimbali kwa njia ya video, vilevile mtandao huo pia umekua msaada kwa makampuni kwani umekua sehemu bora sana ya kufanya matangazo ya biashara ili kufikia watu wengi zaidi wanaoingia kwenye mtandao huo kwaajili ya kuangalia video.

Katika kujua ni video gani yenye dhamani kubwa mpaka sasa kwenye mtandao huo basi hii ndio list ya video kumi ambazo zimeangaliwa sana kuliko video zingine kwenye mtandao maarufu wa Youtube na hatimaye kuwa video zinazo tengeneza hela nyingi kuliko video zote kwenye mtandao huo maarufu wa Youtube. Kumbuka kwa mujibu wa mitandao mbalimbali Youtube inalipa dollar za marekani $1000 kwenye views milioni 1 na hiyo ni mara baada ya kutoa asilimia 45 ambayo inachukuliwa kama ada ya kukupa huduma na kampuni hiyo Google.

1. “See You Again – Wiz Khalifa featuring Charlie Puth – Views Bilioni 2.910 

China Kutumia Roboti Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Corona

Video hii ya Wiz Khalifa inaingiza dollar za marekani $2.9 milioni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 6,490,200,000.00 hii ni baada ya mtandao wa google kuchukua asilimia 45 ya makato yake. Kumbuka kiwango hicho cha Tanzania ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo tarehe 14 hivyo pesa hiyo inaweza kuwa zaidi au pungufu kidogo. Video zingine ni kama zifuatazo.

2. “Gangnam Style – Psy – Views Bilioni 2.897

3. “Sorry – Justin Bieber – Views Bilioni 2.641

4. “Uptown Funk – Mark Ronson featuring Bruno Mars – Views Bilioni 2.552

5. “Despacito – Luis Fonsi featuring Daddy Yankee – Views Bilioni 2.529

6. “Masha and the Bear – Recipe for Disaster Get Movies – Views Bilioni 2.315

7. “Shake It Off – Taylor Swift – Views Bilioni 2.252 

8. “Bailando – Enrique Iglesias ft Descemer Bueno & Gente De Zona – Views Bilioni 2.237

Vodacom Yaja na Huduma ya Malipo ya Kujirudia Kupitia M-Pesa

9. “Sugar – Maroon – Views Bilioni 2.156

10. “Roar – Katy Perry – Views Bilioni 2.134

Na hizo ndio video ambazo ni maarufu sana kwenye mtandao wa youtube na ndio video 10 ambazo zinatengeneza hela nyingi kuliko video nyingine kwenye mtandao maarufu wa Youtube, Kama unataka kujua zaidi unaweza kuangalia list hii ya video zilizo angaliwa sana kwenye mtandao huo hapo mwaka jana 2016.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Wikipedia , Thenextweb

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.