Habari kutoka katika gazeti la mtandaoni la mwananchi zinasema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitoza faini kampuni zote za simu kwa kosa la kusajili laini bila vitambulisho na kutofuata utaratibu.
Kampuni hizo zilizotozwa faini hiyo ni pamoja na kampuni za Airtel ambayo imetozwa faini ya Sh1.08 bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni), Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105 milioni) pamoja na kampuni ya Halotel (Sh1.6 bilioni).
Mwananchi imeendelea kuandika kuwa kwa kunukuu kuwa Mhandisi James Kilaba amesema hapo jana (Julai 14) kuwa hii si mara ya kwanza kwa watoa huduma hao kukiuka sheria hivyo kutokana na kurudia kosa hilo, TCRA imezitoza kampuni hizo faini zaidi ambazo Airtel imetozwa Sh542 milioni, Smart (Sh37 milioni), Tigo (Sh625 milioni), Zantel (Sh52 milioni) na Halotel (Sh822 milioni).
Lakini kama bado haitoshi pia, kampuni hizo zimetozwa Sh500 milioni kila moja kwa kosa la kuathiri na kuhatarisha usalama wa umma na jamii ya Watanzania kwa kusajili laini bila kufuata utaratibu. imeandika gazeti la mtandaoni la mwananchi hapo jana. TCRA sasa imekua makini sana huku ikipambana na makampuni ya simu baada ya siku za karibuni kupiga marufuku matangazo yanayowekwa na makampuni ya simu kwenye miito ya simu.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.
Chanzo : Mwananchi