Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Picha ya Toleo Jipya la Simu Mpya ya Nokia 8 Yavuja

Hii ndio simu mpya ya Nokia inayotarajia kutoka hivi karibuni
Nokia 8 Nokia 8

Nokia ni moja kati ya kampuni za siku nyingi sana za kutengeneza simu, lakini pia hivi karibuni kampuni hiyo ilidhibitisha kuamia kwenye upande wa Android kwa kuanza kutengeneza simu zake zenye kutumia mfumo huo.

Katika kufanikisha hayo kampuni ya Nokia ilitangaza rasmi hapo mwaka 2016 kuwa kampuni ya HMD Global ndio kampuni itakayo shulika na utengenezaji wa simu hizo mpya zenye mfumo wa Android. Hatimaye Nokia kupitia kampuni hiyo imefanikiwa kutoa simu za Nokia 6, Nokia 5 pamoja na Nokia 3 ambazo zote zilitangazwa rasmi huko nchini india.

Advertisement

Kuendeleza mfululizo wa simu hizo hivi karibuni tumesikia na kuona tetesi za kuja kwa simu nyingine kutoka Nokia hapa nazungumzia Nokia 8, Simu hiyo inasemekana kuja na kioo cha inch 5.3 chenye teknolojia ya QHD screen, pamoja na processor ya Snapdragon 835, huku ikiendeshwa na RAM ya GB 4 au GB 6 pamoja na kamera mbili kwa nyuma zilizotengenezwa na Zeiss lenses.

Simu hii ambayo siku ya leo ndio imeonekana picha yake kwa mara ya kwanza inategemewa kutoka rasmi tarehe 31 July huku wateja wa Nokia wakijiweka tayari kupata simu hii kwa bei nafuu kupitia maduka mbalimbali hapa Tanzania na dunia kwa ujumla. Kwa sasa kama unataka kununua simu za Nokia ni vyema kutafuta Nokia 6, Nokia 5 au Nokia 3 kwenye masoko mbalimbali mtandaoni kama vile amazon.com.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : VenturaBeat

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use