“Huenda” Kenya Ikazima Mitandao ya Kijamii Siku ya Uchaguzi

Wakenya wahaswa kutumia vizuri mitandao ya kijamii wakati huu wa uchaguzi
kenya mitandao ya kijamii kenya mitandao ya kijamii

Kiongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya Francis Wangusi amesema kuwa bado hawajafikiria kuzima matumizi ya internet nchini humo lakini wanatoa tahadhari kwa watu kutoku tumia vibaya mitandao ya kijamii nchini humo

Hata hivyo kiongozi wa Tume ya uwiano na utangamano nchini Kenya, Francis Ole Kaparo amesema kuwa ni “vyema baadhi ya mitandao ya kijamii ikazimwa” tume hiyo iliundwa ili kufuatilia maneno ya chuki yanayotolewa na viongozi na raia mbalimbali kipindi cha uchaguzi na hii ni baada ya uchaguzi wa miaka iliyopita kusababisha vurugu huku ukisababisha vifo vya watu zaidi ya 1000 nchini humo.

Huku zikiwa zimesalia siku 19 kabla ya uchaguzi mkuu nchini kenya, wakenya wa matabaka mbali mbali wana wasiwasi hasa kuhusu joto la siasa linaloendelea kupanda kwenye mitandao ya kijamii. Kwenye mkutano na wadau wanaohusika na maandalizi ya uchaguzi mkuu, Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya Francis Wangusi alionya kuwa mitandao inayochapisha habari za uzushi itafungwa.

Advertisement

Hata hivyo Mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano Francis Ole Kaparo kwa upande wake alisema kuwa wanachunguza wasimamizi wa mitandao ya WhatsApp 21 ambayo imekuwa ikichapisha taarifa za uzushi na kwamba uchunguzi unaendelea. Hayo yanajiri siku chache tu baada ya baadhi ya mitandao kuchapisha taarifa za uzushi kuwa rais mstaafu Mwai Kibaki ameaga dunia.

Wakati hayo yakijiri nchini Kenya, shirika la utafiti la Paradigm Initiative Nigeria, limetoa matokeo ya utafiti wake unao onyesha kuwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa ukiukaji wa uhuru wa kujieleza kwenye mitandao ya kijamii.

Ni kutokana na hilo ambapo sekta binafasi nchini Kenya iliwaleta pamoja wadau wanaoandaa uchaguzi kuwahakikishia wawekezaji usalama wao. Serikali imesema kuwa haitakubali watumiaji wa mitandao kuvuruga amani kwa kueneza habari za uzushi. “Waambie wakenya, hakuna mahali wanaweza kujificha hata kwenye mitandao ya kijamii bila ya kutambuliwa. Hatufikirii kufunga mtandao wa inteneti kama vile watu wanavyosema,”alisema Francis Wangusi, mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya, CAK.

Serikali imewekeza dola milioni 5.8 sawa na shilingi milioni 600 za kuchunguza wanaotumia mitandao ya kijamii kwa njia isiyostahili. Wangusi alivionya vyombo vya habari dhidi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya tume ya kusimamia uchaguzi na mipaka kufanya hivyo.

Wasimamizi wa mitandao ya WhatsApp wameonywa dhidi ya kupeperusha habari za uvumi, hata hivyo kulingana na wachambuzi, hatua ya kuwapata wachochezi hao itakuwa vigumu, kwa kuzingatia historia mbovu ya taifa hilo ya kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaohusika na uchochezi wa mitandaoni.

Lakini Francis Ole Kaparo, mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano nchini Kenya, anasema wamezitambua “Group” 21 za WhatsApp ambazo zinaeneza chuki na uchochezi kote nchini na wanaendeela kuwachunguza wasimamizi wa group hizo. “Njia bora za kukabili suala hilo ni kuwatafuta wasimamizi wa mitandao hiyo,” alisema Kaparo.

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 69 ya Wakenya wanatumia mitandao ya kijamii, huku wale wanaotumia simu ikifikia asilimia 74. Serikali nyingi barani Afrika zinafunga mitandao ya kijamii kwa hofu ya watumiaji kueneza uchochezi kwa kufunga mitandao kama ilivyotokea nchini Ethiopia, Uganda na Burundi. Huku Kenya, Tanzania na Rwanda zikiweka sheria kali za kuwadhibiti wanaochochea na kueneza habari za uwongo kwenye mitandao.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Abc News, DW Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use