Sasa Huwezi Kupotea Unapokwenda Microsoft Yakuletea Path Guide

Sasa huu ndio mwisho wa kuuliza unapotaka kwenda
Microsoft Path Guide Microsoft Path Guide

Wote tunajua usumbufu unaotokana na wewe au mtu yoyote kuuliza mahali unapo taka kwenda iwe ni ndani ya jengo flani au hata hatua chache kutoka ulipo, ndio maana kampuni ya Microsoft imeamua kukuletea Path Guide.

Path Guide ni app ambayo itakusadia kujua maeneo mbalimbali iwe ni ndani au nje ya jengo flani, app hii haitumi GPS, Wi-Fi au radio signals ili kukuelekeza unapokwenda bali app hii inatumia mtu halisi ili kuelekeza unapokwenda. Mtumiaji ataweza kutumia app hii kwa kuwasha app hiyo kisha kurekodi hatua pamoja na njia anazopita kisha ataweza kuziweka wazi ili mtu mwingine kuziona au pia utaweza kumtumia mtu ili kumuelekeza pale unapokwenda kwa kufuata maelezo yaliyopo kwenye kioo cha simu yako.

Kufanikisha hili wanasayansi kutoka Microsoft Research Asia wametengeneza app hii kwa kufanya app hiyo kutumia sensors za kwenye simu yako ili kurekodi njia unazopita mpaka kufikia kiwango cha idadi ya hatua ambazo ndio baadae zinakusadia kujua hatua unazotakiwa ili kufika eneo flani. Vilevile wataalamu hawa wamefanikisha app hiyo kuweza kuweka vitu kama picha, sauti au maelezo ili kuweza kumsadia mtu anapokua anapita sehemu kadhaa.

Advertisement

App hiyo mpya pia inakupa nafasi ya kuweza kujua sehemu ambazo tayari zina maelekezo hivy ukiwa karibu najengo lenye maelekezo tayari basi app hiyo itakuletea taarifa ili kujua kuna ramani tayari. Kwa sasa unaweza kudownload app hii kupitia Play Store au bofya hapo chini kisha anza kuelekeza marafiki zako mahali unapotaka kwa njia ya kisasa kabisa.

Path Guide
Price: Free

Kwa watumia wa iOS kwa sasa itabidi kusubiri wakati kampuni hiyo ikiangalia mapokeo ya app hii kwa upande wa Android. Kwa habari kuhusu kutoka kwa app hii kwa upande wa iOS endelea kukaa karibu nasi tutaku fahamisha hapa hapa, kwa habari zaidi na jinsi ya kutumia app hii tembelea ukurasa huu.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Microsoft Path Guide

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use