Matangazo Kwenye Miito ya Simu Yakatazwa Rasmi na TCRA

Mamlaka ya mawasiliano imepiga marufuku matangazo kwenye miito ya simu
TCRA-Mhandisi-James-Kilaba TCRA-Mhandisi-James-Kilaba
PICHA NA RAI

Mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania TCRA, siku ya jana ijumaa imetoa tamko kupitia gazeti la mwananchi kuwa sasa matangazo kwenye miito ya simu ni marufuku. Hata hivyo hiyo yote ikiwa ni kutokana na malala miko yaliyotolewa na baadhi ya watumiaji wa simu za mkononi, iimeripoti tovuti ya mwananchi.

Katika taarifa hiyo mwanachi imeandika kuwa TCRA imepiga marufuku matangazo hayo ya biashara yanayowekwa mara mtumiaji anapopiga simu. Aidha TCRA imesema imeamua kufanya hivyo ili kutoa fursa kwa watumiaji wa simu za mikononi kupata mawasiliano bila usumbufu ambao umekuwa ukilalamikiwa

Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema kuwa hadi kufikia siku ya jana (Ijumaa) tayari mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi sana kutoka kwa watumiaji mbalimbali wa simu wakilalamikia kuhusu matangazo hayo yanayotolewa na kampuni za simu. Hata hivyo mkurugenzi huyo amesema tayari TCRA imeshaziandikia barua kampuni zote za simu kusitisha matangazo hayo na itakutana nazo kwa majadiliano ya kina Julai 6 mwaka huu 2017.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Mwananchi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use