Jinsi ya Kulinda Simu Yako ya Android Dhidi ya Virus Mbalimbali

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu mpya ya ulinzi kutoka Google
google play protect app google play protect app

Wote tunajua ulinzi kwenye simu yako ni kitu cha msingi sana, lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo inavyo zidi kuwa ngumu zaidi kulinda simu yako hii inatokana na sababu mbalimbali ambazo zingine hatuwezi kuzuia kwa mfano pale unapo install programu kwenye simu yako.

Hivyo basi leo tutaenda kujifunza jinsi ya kulinda simu yako ya Android ili isiadhiriwe na virusi mbalimbali, njia hii ni bora sana na inafaa kwa watumiaji wa simu zote za Android zenye akaunti ya Google. Lakini kabla ya kuanza ni vyema tujue adhari zinazotokana na simu yako kuadhiriwa na virus mbalimbali, madhara kadhaa yanayotokana na haya ni mengi sana na baadhi ni kama simu yako kuisha chaji kwa haraka, kujua madhara mengine soma makala ya athari za virus kwenye simu yako ya Android au iOS.

Basi moja kwa moja twende tukangalie somo letu la leo, somo hili linatokan na kampuni ya Google kuleta sehemu mpya ya Google Play Protect ambayo imetokana na baadhi ya programu za Android kusemekana kuleta Virusi kwenye simu za Android. Hivyo Google wametengeneza sehemu hiyomaalumu kwaajili ya kulinda simu yako ili isiadhiriwe na virusi kutoka kwenye baadhi ya programu.

Advertisement

Sasa ili kuwasha sehemu hiyo inakuitaji kufuata hatua hizi rahisi sana ambazo zitakusaidia sana kulinda simu yako. Hatua ya kwanza ingia kwenye Settings au tafuta programu iliyo andikwa Google Setting kwenye simu yako ya Android kisha tafuta mahali palipo andikwa Security kisha chagua Google Play Protect kisha bofya sehemu iliyo andikwa Scan device for security threats baada ya hapo utakuwa umewasha sehemu hiyo ambayo itakuwa inalinda simu yako masaa yote unapo install programu yoyote.

Mpaka hapo utakuwa umewezesha simu yako kuwa salama na kuzuia virusi vinavyotokana na programu mbalimbali, kumbuka ili kuwa salama zaidi usi – install programu kutoka sehemu nyingine nje ya soko la Play Store.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Google Play Protect

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use