Kama Umezoea Kutumia Simu Ukiwa Chooni Soma Hii

Kama unayo tabia hii ni vyema kujufunza kuiacha mara moja.
simu chooni simu chooni

Hii ni moja kati ya tabia ambayo kama unayo basi huna budi kujifunza kuiacha mara moja, kwani wataalamu kutoka marekani katika utafiti wao wamesema kuwa simu yako inabeba wadudu wa chooni zaidi kuliko hata choo chako.

Watafiti hao kutoka marekani walisema kuwa kutokana na utafiti huo wamegundua kuwa tabia hii ni kubwa sana miongoni mwa watumiaji wa simu za mkononi, kwani utafiti huligundua kuwa asilimia 90 ya watu wanaotumia smartphone wanazitumia pia wakiwa chooni.

Hata hivyo katika makala ya utafiti huo ya mwaka 2011 kutoka shule ya Hygiene & Tropical Medicine ilisema kuwa katika kila simu sita mabazo zilifanyiwa utafiti basi simu moja lazima inakua na chembechembe za uchafu unaotokana na vyoo au mabafu.

Advertisement

Kwa hapa kwetu tanzania utafiti huu haujafanyka lakini ni wazi sana tabia hii ni kubwa sana miongoni mwetu tena hasa kwenye vyumba zenye vyoo vya kukaa, “ukweli kabisa tabia hiyo sio nzuri sana na unaitajika kujitahidi kuiacha maana chooni kuna wadudu wengi sana ambao ni wabaya sana kwa afya yako” alisema mwandishi wa kitabu cha The Germ Files alipokuwa anahojiwa na gazeti la USA Today.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : The Star Online

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use