Internet Yarejea Tena Somalia Baada ya Kukatika Kwa Siku 3

Baada ya kukatika kwa internet kwa takriban zaidi ya wiki tatu
INTERNET SOMALIA INTERNET SOMALIA
PICHA NA DW SWAHILI

Habari kutoka kwenye mtandao wa DW Swahili zinasema kuwa, huduma za mtandao wa intaneti zimerejea nchini Somalia baada ya kukatika kwa zaidi ya wiki tatu na kuigharimu nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kiasi cha dola milioni 10 kwa siku, wamesema maafisa nchini humo.

Hormuud Telecom, kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano nchini Somalia, ilitangaza kurejeshwa kwa huduma ya mawasiliano kupitia ujumbe mfupi kwa wateja wake. Kukatika kwa huduma za intaneti kulisababisha ghadhabu nchini Somalia kote na kuathiri maeneo ya kati na kusini mwa nchi, hiyo ukiwemo mji mkuu wa Mogadishu. Serikali iliutaja ukatikaji huo kuwa ni janga kubwa hata hivyo Maafisa na watoaji wa huduma za intaneti wamesema tatizo hilo lilisababishwa na meli ya kibiashara iliyokata kebo ya chini ya bahari.

Makampuni makubwa yameripoti hasara ya mapato inayofikia mamilioni ya dola. Shughuli za vyuo vikuu zilivurugwa pia na ukatikaji huu wa huduma ya intaneti. Pia ulitatiza juhudi za kukabiliana na ukame uliolikumba taifa zima na kuwafanya kiasi nusu ya raia milioni 12 wa taifa hilo kuhitaji msaada wa chakula.

Advertisement

Hata hivyo hivi leo wakazi wa mji mkuu huko nchini somalia walisherehekea kurudi kwa huduma hiyo na mmoja wao kunukuliwa na DW akisema “Hii ni habari njema kweli. Tumekabiliwa na wiki kadhaa za kukatika kwa huduma ambazo zimeathiri biashara zetu vibaya sana,” alisema Ahmed Mohamed, meneja wa kampuni ya usafiri ambayo ililaazimika kufunga shughuli zake wakati wote huduma hiyo ilipokuwa haipatikani.

Ukosefu wa huduma za intaneti uliwakwamisha pia wagonjwa waliokuwa wanatafuta matibabu nje ya nchi kutokana na kushindwa kukamilisha nyaraka za mtandaoni. “Baba yangu alikwama Mogadishu kutokana na kukatika kwa mtandao. Sasa tunaweza kumpeleka India baada ya kupokea nyaraka zote za kitabibu kupitia mtandaoni,” alisema Nur Hussein, imeripoti tovuti ya DW Swahili.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : DW Swahili

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use