in

Instagram Yaleta Njia Mpya ya Kutoa Maoni Kwenye Stories

Instagram yaja na njia mpya ya kujibu maoni kwenye Stories

Instagram stories

Mtandao wa instagram kupita programu zake za instagram za iOS na Android hivi karibuni zimefanyiwa mabadiliko mbalimbali, mabadiliko hayo ambayo yamewezesha watumiaji kutumia programu hiyo tofauti sasa yanaongezwa zaidi kwa kuletwa njia mpya ya kureply au kujibu picha na video kwenye sehemu ya stories kwa kutumia picha na video.

Jinsi ya kutumia sehemu hiyo ambayo sasa imeshatoka kwenye app za android na iOS ni rahisi sana, unachotakiwa ni kubofya kitufe cha kamera kinacho onekana wakati unaangalia video ya mtu kupitia kwenye stories, baada ya hapo utapelekwa kwenye sehemu maalumu ambapo utaweza kurekodi video au kupiga picha pia utaweza kuweka sticker na filter mbalimbali kabla ya kutuma picha yako kama maoni kwa mtu unaye angalia storie yake kupotia sehemu hiyo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hata hivyo mtumiaji atapata picha yako kupitia sehemu ya meseji kwenye app hiyo ya instagram na kama ilivyo sehemu ya stories picha au video hizo zitakaa kwa muda wa masaa 24 tu. Sehemu hiyo kwa sasa tayari iko kwenye app za instagramu za mifumo yote ya Android na iOS cha msingi update app yako sasa na utapata sehemu hiyo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video

Instagram Yaleta Njia Mpya ya Kutoa Maoni Kwenye Stories
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.