in

Video : Hizi Ndio Simu Tano Bora Mpaka Sasa Mwaka 2017

Simu ipini bora kwa thamani ya pesa yako.? Basi soma list hii hapa

Simu Bora 2017

Mpaka sasa tayari tumefikia nusu mwaka na tayari tumeshaona simu mbalimbali ambazo zimezinduliwa ndani ya muda huo, lakin je simu zipi ni bora sana mpaka sasa na je ni simu gani ambayo inaweza kuendana na dhamani ya pesa yako.? Basi ifuatayo ndio list ya simu tano bora hadi kufikia sasa ndani ya mwaka huu yani 2017.

No 5. Huawei P10

Moja kwa moja twende tukanze na namba tano ambayo imeshikwa na simu kutoka kampuni ya Huawei hapa nazungumzia simu mpya ya Huawei P 10, simu hii ni moja kati ya simu zenye uwezo mkubwa sana wa kamera kwani simu ina kamera mbili za leica zenye uwezo mkubwa sana kujua sifa kamili soma ukurasa huu.

No 4. HTC U11

Kwenye namba nne ni simu ya kisasa kabisa HTC U11 simu hii ni moja kati ya simu zenye teknolojia ya hali ya juu pamoja na sifa bomba sana zenye kukupa kile unacho staili, simu hii inakuja na teknolojia ya kipekee ya kugusa kwa pembeni teknolojia ambayo inapatikana pekee kwenye simu hiyo mpaka sasa kujua zaidi tembelea ukurasa huu.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A21s

No 3. BlackBerry KEYone

Blackberry Keyone ni moja kati ya simu ambazo zimejitahidi sana kuja kwa njia ya tofauti simu hii pamoja na kuwa na matatizo mwanzoni mwa kutoka kwake lakini simu hii ni moja kati ya simu bora sana na yenye nguvu sana, simu hii iliyozinduliwa miezimichache iliyopota sasani moja kati ya simu bora sana duniani. Kama unataka kujua sifa zake tembelea ukurasa huu.

No 2. LG G6

Namba mbili kwenye list hii inashikwa na simu bora yenye teknolojia ya kisasa yaani LG G6 simu hii ni mojakatiya simu kali sana sana, simu hii inakuja na uwezo wa hali ya juu sana uku ikikupa uwezo wa kutumiasimu yako kwa namna ya tofauti kupitia kioo bora chenye teknolojia ya Fullvision usisikilize maneno yangu soma hapa mwenyewe hapa sifa za simu hii bora.

No 1. Samsung Galaxy S8/S8+

Namba moja tunakuatana na Samsung Galaxy S8, simu hii ni bora sana na ni moja kati ya simu zilizo tengenezwa kwa ubora sana huku ikikupa sifa za kisasa sana. Kama kawaida Samsung wamefanikiwa tena kuleta simu ambayo imekidhi matakwa ya wateja wake, ukweli ni kwamba ukipata au ukitumia simu hii ndio utakuja kwa Samsung Galaxy S8 ni simu bora sana kwako. Unaweza kusoma sifa kamili za simu hii kwa kupitia ukurasa huu hapa.

Update : Soma hizi hapa simu bora kwa mwaka mzima 2017

Na hizo ndio simu tano bora mpaka sasa, kumbuka bado tunaendela kusubiri kutoka kwa simu mpya ya iPhone 8 pamoja na Galaxy Note 8 ambazo zote ziko mbioni kutoka miezi ya karibuni, tutaongeza list hii pale tutakapo ona uwezo wa simu hizo. Lakini unaweza ukatuambia kama simu simu gani inaweza kuingia kwenye list hii kupitia maoni yako hapo chini.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Reno 4 na Reno 4 Pro

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 1

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.