Costech Yahasa Taasisi za Fedha Kukumbuka Wataalam wa Tehama

Ni muda sasa wa Tehama kupewa kipaumbele na Taasisi za fedha
TEHAMA TEHAMA
PICHA NA ZANZINEWS

Katika hali ya kuendeleza teknlojia ya habari na mawasiliano,tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), imezitaka taasisi za fedha nchini kuziona fursa zilizopo kwa wabunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kuwawezesha mitaji limeripoti gazeti la mwananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Costech, Dk Hassan Mshinda alisema hayo alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, Alisema taasisi za fedha zimejielekeza zaidi kwenye miradi ya bidhaa au huduma zinazoonekana na kuisahau sekta hiyo ndogo inayokua kwa kasi.

“Watu wa benki hawaelewi chochote kuhusu ubunifu unaofanywa huku, hivyo kutoziona fursa zilizopo. Wabunifu hawa wana mawazo yanayoweza kutoa matajiri endapo watawezeshwa kwa mitaji midogo wanayoihitaji kwa kianzio,” alisema Dk Mshinda kupitia gazeti la mwananchi.

Advertisement

Hata hivyo Kituo cha Bun Hub kilichopo Costech kinatoa fursa kwa wabunifu wa programu zinazotatua kero mbalimbali zilizopo kwenye jamii kwa kutumia Tehama. Ndani ya miaka mitano iliyopita, zaidi ya vijana 5,000 wamewezeshwa, kampuni 300 za kibunifu zimeanzishwa, miradi 68 imetekelezwa na zaidi ya wanafunzi 450 wa vyuo vikuu wamepewa mafunzo ya vitendo. Mwanzilishi wa Bun Hub, Jumanne Mtambalike alisema endapo eneo hilo litatazamwa vizuri na wadau wakalipa kipaumbele, Tanzania itakuwa na mabilionea wengi baada ya muda mfupi.

“Kampuni za kibunifu ni biashara kubwa inayohitaji umakini kuisimamia. Vijana waliopo huku wana mtazamo wa mbali wanapoandaa programu zao zinazoweza kutumika kimataifa. Wanahitaji kushikwa mkono wanapoanza,” alisema Mtambalike ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Sahara Ventures.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Mwananchi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use