Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apple Yatoa Toleo Jipya la iOS 10.3.3 Download Link Ziko Hapa

Kama wewe unatumia iPad, iPhone na iPod soma hii nimuhimu kwako
iOS 10.3.3 iOS 10.3.3

Kampuni ya Apple imetoa rasmi toleo jipya la iOS 10.3.3 kwaajili ya iPhone, iPad pamoja na  iPod Touch, toleo hili jipya ambalo limetoka hapo jana linakuja na ukarabati mbalimbali wa mfumo wa zamani wa iOS 10.3.

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes mfumo huu mpya utakujana na marekebisho machache pamoja na marekebisho ya ulinzi uliotokana na matatizo mbalimbali ya mfumo uliopita wa iOS10.3, hata hivyo toleo hilo ni maandalizi ya toleo jipya kabisa la iOS 11 ambalo limepangwa kuja hivi karibuni na kama tulivyoona toleo hilo jipya litakuja na vitu kibao kama vile emoji mpya na mengine mengi sana ambayo yaliotangazwa nakampuni ya Apple.

Advertisement

Kwa sasa kama unataka kupakua toleo hili jipya la sasa la iOS 10.3.3 unaweza kutumia programu ya iTune au kwa namna nyngine unaweza kuingia kwenye sehemu ya “Settings” kwenye kifaa chako kisha chagua kwa kubofya “General” alafu bofya sehemu ya “Software Update”. Baada ya hapo utaona toleo hilo jipya la iOS 10.3.3.

Lakini kama njia zote hizo zimeshindikana basi usijali unaweza kutumia link maarufu kama (IPSW Download Links) ambazo zitakusadia kudownload toleo hilo jipya kisha utatumia iTune kuinstall kwenye kifaa chako, muhimu ni kuchagua link kutokana na aina na toleo la kifaa chako.

Kumbuka kuwa makini sana kuchagua aina ya link kutokana na aina ya kifaa chako, njia inasemekana kuwa njia ya kitaalamu kidogo lakini sio ngumu hivyo kama unaona umeshinda kutumia njia hii unaweza kutazama video hapo chini jinsi ya ku-install.

Vile vile kampuni hiyo leo imetoa matoleo mapya ya macOS, watchOS pamoja na tvOS yote yakiwa na lengo la kuongeza ulizi na kurekebisha baadhi ya matatizo hivyo unaweza kuangalia update kwenye kompyuta yako sasa au kifaa chako cha Apple.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Forbes, OSX Daliy

4 comments
  1. Kila nikijaribu ku update simu yangu inaniambia iko up to date lkn cha ajabu natumia iphone 4s na version yake bado iko chini sana ni 9

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use