Apple Yatangaza Kuleta Aina Mpya za Emoji Hivi Karibuni

Hizi ndio baadhi ya emoji mpya zinazotarajiwa kwenye vifaa vya Apple
emoji emoji

Apple imedhibitisha kuleta aina mpya ya emoji ambazo zitakuja kwenye vifaa vipya vya Apple vitakavyotoka mwaka huu, kama bado hujaziona emoji hizo, basi hizi ndio emoj zenyewe ambazo zilitumwa na kwa mara ya kwanza na CEO wa Apple masaa machache yaliyopita kwenye akaunti ya Twitter.


Emoji hizo ni kama vile zombies, fairies, breastfeeding mother, pamoja na exploding head zote zikiwa ni toleo jipya la Unicode 10 emoji. Hizo ni baadhi tu ya emoji ambazo zinategemewa kuja kwenye vifaa vya Apple, kujua list ya majina yote ya emoji hizo soma hapa.

Hata hivyo emoji hizo zinategemewa kuja kwenye vifaa vinavyo tumia iOS, macOS, pamoja na watchOS. Apple inasherekea World Emoji Day kwa kutoa emoji hizo pamoja na kuonyesha baadhi ya majina ya filamu kwenye iTune kwa kutumia emoji mbalimbali.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Apple Newsroom

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use