WhatsApp Yaongeza Photo Filter na Albums Kwenye Mfumo wa iOS

Whatsapp yaongeza sehemu mpya kwenye programu yake ya mfumo wa iOS
WhatsApp ya iOS WhatsApp ya iOS

Kama wewe ni mtumiaji wa simu zenye mfumo wa iOS basi hii ni habari njema kwako kwani hapo jana WhatsApp ilianza kutoa toleo lake jipya lenye sehemu mpya ndogo, sehemu hizo ni Photo Filter pamoja na Albums.

Kwa upande wa sehemu ya album sasa utakuwa ukituma picha zaidi ya tano picha hizo zitajiweka kwenye mfumo wa album ili kukupa urahisi na nafasi ya kujua picha hizo zilitumwa kwa pamoja. Pale utakapo gusa picha moja ndipo itaweza kujaa kabisa kuwa picha moja.

Pia kwa jinsi inavyonekana whatsapp inataka kuwekwa kama facebook kwani sasa WhatsApp imeongezwa sehemu ya filter kwenye sehemu ya kamera, kwa sasa ziko filter za aina tano lakini inategemewa filter hizo kuongezwa kadri siku zinavyokwenda, filter hizo zinafanyakazi kwenye video, Gif na hata kwenye picha.

Advertisement

Kwa sasa bado hakuna taarifa kuhusu sehemu hiyo kuja kwenye mfumo wa Android, lakini bila shaka sehemu hizo zitakuja ziku sio nyingi. kupata taarifa ya sehemu hiyo itakapo kuja kwenye Android endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video. 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use