Mtandao wa Snapchat Waleta Sehemu Mpya ya Snap Map

Sasa snapchat yaja na sehemu mpya inayoitwa snap map
snap map snap map

Kampuni ya snap Inc kupitia programu yake ya snapchat leo imezindua sehemu yake mpya inayoitwa snap map, sehemu hiyo ambayo inaleta uwezo wa kutumia programu hiyo kwa namna mpya imezinduliwa rasmi siku ya jana na sasa inapatikana kwenye programu za mifumo yote ya Android pamoja na iOS.

https://www.youtube.com/watch?v=bvl82FfnUvw

Sehemu hiyo itakupa uwezo wa kujua nini kinatokea popote ulipo kwa kutumia ramani maalumu iliyoko kwenye programu hiyo ya snapchat, akielezea jinsi inavyofanya kazi kupitia mtandao Refinery29 Jack Brody, Mtengenezaji bidhaa wa kampuni ya snapchat alisema unapo update programu ya snapchat utapelekwa kwenye hatua chache ambazo zitakuwa zikikuelekeza jinsi ya kuingia kwenye snap map na baada ya hapo utatakiwa kuwasha sehemu maalumu ya location ili uweze kutumia sehemu hiyo kisha utaweza kuchagua ulipo alafu moja kwa moja utaruhusu mahali ulipo kuonekana na marafiki baadhi au marafiki wote hiyo inategemea na wewe kisha hapo utakuwa uko tayari kutumia sehemu mpya ya snap map.

Advertisement

Hata hivyo sehemu hiyo mpya itakupa uwezo zaidi wa kujua mahali kwenye matamasha mbalimbali kwa kutumia ramani hiyo, akielezea tena sehemu hiyo inavyofanya kazi mtengenezaji bidhaa wa snapchat alisema kwenye maojiano yake na mtandao wa Refinery29 kuwa, kwa kutumia snap map unaweza kujua kinachoendelea kwa marafiki zako lakini pia unaweza kujua nini kinachotokea kwa kutumia sehemu hiyo, kwa kutumia sehemu hiyo snap map inauwezo wa kuonyesha sehemu yenye tamasha au mkusanyiko wa watu wengi kwa kutumia “map heat” hii ikionyesha watu wengi wanaotumia snapchat walipo kwa pamoja hivyo kukupa urahisi wa kujua mahali penye matamasha na mikusanyiko ya watu ambayo pengine ni muhimu kwako.

Sehemu hiyo mpya kwa sasa tayari inapatikana kwenye programu zote za snapchat unaweza ku-update ili kupata sehemu hiyo na kuanza kushriki na marafiki zako sehemu ulipo. Kama huna programu hiyo ya snapchat basi ni wakati wa kudownload sasa..

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use