Simu Mpya za Nokia 6, Nokia 5 na Nokia 3 Zatoka Rasmi Uko India

Nokia watoa simu zake zingine zenye kutumia mfumo wa Android
nokia_3_nokia_5_nokia_6 nokia_3_nokia_5_nokia_6

HMD Global kampuni iliyopewa mamlaka na kampuni ya Nokia kutengeneza na kusambaza simu zake mpya, hivi karibuni imezindua simu mpya za Nokia 6, Nokia 5 pamoja na Nokia 3.

Kama hapo awali tulivyona awali simu hizi zilionekana kwenye mkutano wa CES na baadae simu ya Nokia 6 kuzinduliwa rasmi. Kwa siku za karibuni kampuni ya Nokia kupitia kampuni yake ya usambazaji ya HMD Global sasa imezindua simu zake mpya tatu za Nokia 6, Nokia 5 pamoja na Nokia 3 huko nchini india.

Kwa undani sifa za Nokia 6 unaweza kupata na kuzisoma kupitia ukurasa huu, sifa za Nokia 5 pamoja na Nokia 3 ni kama zifuatazo. Kwa upande wa Processor Nokia 5 inatumia processor ya 1.4GHz octa-core Qualcomm Snapdragon 430 processor clubbed yenye Adreno 505 GPU, wakati Nokia 3 inakuja na processor ya 1.4GHz quad-core Mediatek MT6737 processor yenye Mali-T720MP2 GPU.

Advertisement

Kwa upande wa RAM simu hizi mbili za Nokia 5 pamoja na Nokia 3 zinakuja na uwezo wa kawaida wa RAM ya GB 2, kwa upande wa ukubwa wa ndani simu hizi zinakuja na ukubwa wa ndani unaofanana wa GB 16 na unaweza kuongeza ukubwa huo kwa kutumia Memory Card ya hadi GB 120.

Na kwa upande wa vioo vya simu hizi za Nokia 5 pamoja na Nokia 3, Nokia 5 inakuja na kioo cha ukubwa wa inch 5.2 ikiwa na uwezo wa pixel 720 na Nokia 3 inakuja na kioo cha inch 5 nayo pia ikiwa na uwezo wa pixel 720 kwenye kioo chake. Kwa upande mwingine wa kamera simu hizo zinakuja na uwezo wa megapixel 13 kwa Nokia 5 uku ikiwa na teknolojia za f/2.0 aperture, Phase Detection Autofocus pamoja na dual-LED flash. Tukihamia kwa Nokia 3 simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 8 huku ikiwa na teknolojia za f/2.0 aperture, autofocus pamoja na LED flash.

Kwa upande wa kamera za mbele yaani (Selfie Camera) simu hizi zote mbili za Nokia 5 pamoja na Nokia 3 zinakuja na kamera ya megapixel 8. Vitu vyote kwenye simu hii vitakuwa vikiendeshwa na toleo jipya la mfumo wa Android ambao utakuwa na ulinzi zaidi pamoja na usalama wa hali ya juu, hiyo ni kwa mujibu wa HMD Global kampuni ya usambazaji na utengenezaji wa simu za Nokia.

Kuhusu Battery simu hizi inasemekana zinakuja na battery zenye uwezo wa kudumu muda mrefu na chaji zikiwa na uwezo wa 3,000mAh kwa Nokia 5 na kwa upande wa Nokia 3 simu hiyo inakuja na uwezo wa battery wa 2,650mAh. Kwa Upande wa Bei Nokia 5 inasemekana kuja kwa bei ya india Rs 12,899 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 448,861.60 bila kodi na Nokia 3 ikiuzwa kwa Rupia ya india Rs 9,499 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 330,547.82 bila kodi.

Kwa upande wa Tanzania Hapa bado simu hii haijafika ila inawezekana kufika hivi karibuni hivyo kaa tayari kuinunua simu hizi kwenye maduka mbalimbali ya hapa Tanzania. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use