Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa simu za Android basi ni muhimu sana kusoma makala hii na ni vizuri umepata makala hii ili kuweza kujua yale ya muhimu kuhusu mfumo huo wa simu yako yani Android. Hivyo basi kama kwa muda sasa umekuwa ukisumbuliwa na matangazo usiyoyaelewa basi hii ndio sababu…
Kwa muda sasa toka mwezi wa Tano (May) kumetangazwa habari ya Malware mpya ambazo zinaingia kwenye mfumo wa simu yako ya Androd kupitia soko maarufu la Play Store, habari hizi zilitolewa na kampuni ambayo inafanya utafiti wa virus na malware mbalimbali mtandaoni inayoitwa Check Point. Hawa jamaa walifanya uchunguzi na kugundua kuwa kuna aina hiyo mpya ya malware ambayo inatwa Judy Malware.
Judy Malware ni aina ya virusi ambayo inapatikana au inangia kwenye simu yako kupitia baadhi ya programu (App) za android ambazo ziligunduliwa na kampuni hiyo. Hata hivyo wataalamu hao waliweza kujua jinsi malware hizo zinavyofanya kazi, Katika ripoti yake kampuni hiyo ilisema kuwa malware hizo zinapoingia kwenye simu yako zinafanya matangazo kuwepo kwenye simu yako na inachofanya kikubwa ni kubonyeza matangazo hayo yenyewe ili kutengeneza pesa kwa watu walio tengeneza malware hizo, hivyo kupelekea matangazo kuwa mengi sana kwenye app hizo ambazo zimeadhiriwa na Malware hao maarufu kama Judy.
Aitha katika ripoti hiyo kampuni ya checkpoint ilisema kuwa malware hizo hazichukui kitu chochote kutoka kwenye simu yako bali inachofanya ni kuongeza matangazo kwenye simu yako na kupelekea simu yako kuisha chaji haraka kama nilivyo elezea kwenye makala ya sababu za simu yako kuisha chaji haraka, lakini pia haimaanishi kuwa malware hizo sio hatari kwani zimeweza kupita uchunguzi wa Google japo kuwa Google inatumia anti malware na anti virus zenye uwezo wa hali ya juu sana lakini kwenye malware hizi kampuni hii imeshindwa kugundua app hizo.
Hata hivyo kampuni ya Check Point iliweza kuendelea zaidi na kusema programu nyingi zenye malware hizo zimetengenezwa na kampuni ya Korea ambayo imesajili jina lake kwenye soko la Play Store kama ENISTUDIO corp, kampuni inayotengeneza programu za mifumo yote ya Android pamoja na iOS. Kampuni hiyo iliongeza kuwa iliweza kutoa taarifa kwa Goole kuhusu kampuni hii na Google imefanya hatua za kuondoa programu hizo lakini bado kampuni hiyo imetadharisha watumiaji wa andoid kuwa makini na kuto kudownload programu zifuatazo.
- Fashion Judy: Snow Queen style
- Animal Judy: Persian cat care
- Fashion Judy: Pretty rapper
- Fashion Judy: Teacher style
- Animal Judy: Dragon care
- Chef Judy: Halloween Cookies
- Fashion Judy: Wedding Party
- Animal Judy: Teddy Bear care
- Fashion Judy: Bunny Girl Style
- Fashion Judy: Frozen Princess
- Chef Judy: Triangular Kimbap
- Chef Judy: Udong Maker – Cook
- Fashion Judy: Uniform style
- Animal Judy: Rabbit care
- Fashion Judy: Vampire style
- Animal Judy: Nine-Tailed Fox
- Chef Judy: Jelly Maker
- Chef Judy: Chicken Maker
- Animal Judy: Sea otter care
- Animal Judy: Elephant care
- Judy’s Happy House
- Chef Judy: Hotdog Maker – Cook
- Chef Judy: Birthday Food Maker
- Fashion Judy: Wedding day
- Fashion Judy: Waitress style
- Chef Judy: Character Lunch
- Chef Judy: Picnic Lunch Maker
- Animal Judy: Rudolph care
- Judy’s Hospital:pediatrics
- Fashion Judy: Country style
- Animal Judy: Feral Cat care
- Fashion Judy: Twice Style
- Fashion Judy: Myth Style
- Animal Judy: Fennec Fox care
- Animal Judy: Dog care
- Fashion Judy: Couple Style
- Animal Judy: Cat care
- Fashion Judy: Halloween style
- Fashion Judy: EXO Style
- Chef Judy: Dalgona Maker
- Chef Judy: ServiceStation Food
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, kama ume install moja ya programu hapo juu basi ondoa haraka programu hiyo na kutokana na kwamba hakuna njia ya kuondoa malware hao kwenye simu basi ni lazima kufanya format ya simu yako moja kwa moja. Kama unataka kusoma taarifa kamili inapatika kupitia ukurasa huu.
Basi hiyo ndio taarifa ambayo nimeona nikusogeze kwani naona ina uzito ukitegemea malalamiko ya simu kupata moto au kuisha chaji yamekuwa mengi, pengine hii ndio sababu. Haya basi Ili kuhakikisha upitwi na habari za muhimu kama hizi hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku, kumbuka pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.