Sasa Utaweza Kutuma Mafaili ya Aina Zote Kupitia WhatsApp

Sasa kupitia programu ya whatsapp utaweza kutuma file lolote
whatsapp programu whatsapp programu

Kwa wapenzi wa programu ya whatsapp sasa mtaweza kutumia programu ya whatsapp kwa namna ya tofauti kwani sasa mtaweza kutuma mafile ya aina yoyote kupitia programu hiyo maarufu duniani kwa kuchat.

Kupitia programu hiyo sasa utaweza kushare file la aina yoyote lenye ukubwa wa MB 128 kwa mfumo wa iOS na MB 100 kwa mfumo wa Android, hizi ni baadhi ya tweet ambapo watu mbalimbali wameonyesha jinsi wanavyotuma ma-file ya aina ya apk kwa kutumia programu hiyo ya whatsapp.\

Sasa sehemu hiyo inapatikana kupitia programu ya whatsapp beta ambayo unaweza kujiunga na app hiyo kupitia Play Store kwa kutumia link hii hapa kisha ondoa programu yako ya kawaida ya whatsapp kisha download programu ya WhatsApp Beta na utapata sehemu hiyo pamoja na nyingine mpya zitakazokuja.

Kwa sasa kama unataka kutuma file lolote kwa kutumia programu yako ya kawaida ya whatsapp basi fuata maelekezo haya kwenye makala hii HAPA.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use