Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Paypal ili Kufanya Manunuzi Mtandaoni

Fuata hatua hizi kama unataka kujiunga na akaunti ya paypal Mtandaoni
paypal paypal

Kwa muda sana nimepata ripoti mbalimbali kuhusu watu mbalimbali kutaka kufanya manunuzi ya mtandaoni lakini wengi wao wakishindwa kutokana na kutokua na vitu mbalimbali, moja ya vitu hivyo ambavyo tutangalia leo ni akaunti ya malipo ya paypal.

Kwa wasio jua Paypal ni mtandao ambao kazi yake ni kurahisisha malipo kati ya mununzi na muuzaji wa bidhaa au huduma flani kupitia kwenye mtandao. PayPal Holdings, Inc ndio moja ya kampuni za siku nyingi sana ambazo zinawezesha kwa wingi ulipaji kupitia mtandaoni.

Advertisement

Hivyo basi kutokana na hilo mara nyingi kama unataka kununua kitu kwenye mtandao unakutana na njia ya kupia ya paypal hivyo kama huna akaunti hiyo inakuwa ni ngumu sana wewe kuweza kukamilisha manunuzi hayo, ndio maana leo tunakuletea hatua kwa hatua jinsi ya kujiunga na akaunti ya paypal na kwa kuanza ni lazima kusoma mahitaji yafuatayo.

Wezesha Kadi yako ya Bank na Huduma ya Internet Banking

  • Kitu cha kwanza na cha muhimu ni lazima uwe na kadi ya bank (ATM Card) inaweza kuwa CRDB au bank yoyote yenye kutoa huduma za internet banking, hapa kumbuka nilazima kuomba huduma hii kuwezeshwa kwenye kadi yako sio kila kadi inayo huduma hii bali ni lazima kuomba huduma hii pamoja na kujaza fomu maalumu, bank nyingi hapa Tanzania zinafanya huduma hii bure kabisa hivyo ni rahisi kupata huduma hii.

Hakikisha Akaunti Yako ina Kiwango Cha Pesa Angalau Tsh 10,000

  • Baada ya kadi yako kuwezeshwa na huduma ya internet banking au uwezo wa kufanya manunuzi mtandaoni basi hakikisha kwenye akaunti yako ya bank kuna kiasi kisicho pungua dollar 2 ambayo ni sawa na shilingi 6,000 au kuendelea, kifupi unaweza kuweka hata shilingi elfu kumi kwaajili ya kujiunga na huduma hii, hela hiyo haita tumika hivyo usiwe na wasiwasi.

Hakikisha unakuwa na Barua Pepe (Email) Unayo-iamini kwa Asilimia 100

  • Hakikisha unakuwa na kadi yako ya bank wakati unafanya hatua hizi za kujiunga pia ni mhumu sana kuwa na barua pepe ambayo unaweza kuwa na uwezo wa kuifungua muda wowote, hii ni muhimu sana kwani huduma ya paypal inategemeana na barua pepe kwa kiasi kikubwa sana.

Hakikisha Unakuwa na Namba ya Simu Unayoiamini 

  • Kitu cha muhimu cha mwisho ni kuwa na namba ya simu ambayo una-iamini sana na ambayo unakuwa nayo wakati wote hii ni muhimu sababu inasaidia ulinzi kwenye akaunti yako pamoja na kukupa uwezo wa kurudisha akaunti yako pale inapopotea hii ni muhimu sana.

HATUA ZA KUFUATA

Baada ya kuhakikisha unavyo vitu vyote hapo juu basi endelea kwa kufuata hatua hizi kama ilivyo kwenye ukurasa huu ni muhimu kuzingatia kila hatua kama ilivyo.

Baada ya kufuata maelezo hayo kwenye video basi utakua umefanikisha kujiunga na akaunti ya paypal kitakacho tokea ni kwamba hakikisha una hakiki akaunti yako baada ya kujisajili, kuji hakiki huko unatakiwa kuingia kwenye barua pepe yako na utakuta email kisha bofya Confirm kisha utakuwa umemaliza hatua hiyo.

Kingine muhimu kwenye akaunti yako kutakatwa dollar moja $1 ambayo itachukuliwa ili kufanya uhakiki wa kadi yako kisha baada ya hapo hela hiyo itarudishwa kwenye akaunti yako, baada ya kufanya hatua zote hizi basi utakuwa uko tayari kufanya manunuzi mtandaoni kwa kutumia akaunti yako ya Paypal. Kumbuka tu email barua pepe yako pamoja na password.

Kama utakuwa umekwama sehemu yoyote usisite kutuandikia kwenye sehemu ya maoni hapo chini, pia unaweza kutuandikia kupitia akaunti zetu zote za mitandao ya kijamii na tuta kusaidia moja kwa moja kwenye mitandao hiyo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video

30 comments
    1. Habari Somido, Unaweza kutoa kwenda kwenye akaunti yako ya bank kwa kutumia kadi yako ya Master Card lakini ni lazima akaunti yako iwe verified.

  1. Samahani naombeni mnieleweshe kwa mfano nataka kutengeneza app itakayoweza kufanya kazi kama ant virus napo hatua ndo hizo ?

  2. Je hakuna gharama zozote ambazo paypal wanakata katika akaunt ya mteja kama gharama za uendeshaji, pi je kila mtu anapofanya manunuzi mtandaoni, kunamakato yeyote Paypal wanakata?

  3. ninajaribu kufungua paypal account for a long time now ambayo inaweza kureceive pesa….please help me out!

  4. Maoni*ndugu wanatechn naomba kufahamu Namna ya kujua kuwa nimeuza picha yangu Foap na Namna ya kupata fedha zangu.

  5. Asante sana kwa maelezo mazuri
    Ila kuna vitu sijaelewa kwanza video haiplay hivyo sijaona maelezo yaliopo kwenye video
    Pili nilifanya utaratibu wote kama nilisoma hapo lakini sijaona tofauti yoyote maana mwanzo iligoma na sasa bado inagoma kukubali credit card sasa sijajua ni bank niliyofungulia account ndo inazingua au ni mm nakosea

  6. Habry Mkuu.!?
    Naomba msaada jinsi nitaweza ku withdrawal money ya$
    Kwa njia ya bank,PayPal,Bitcoin na credit card,,,,,,,.Nimetengeneza pesa online ila njia za kuitoa ndio ngumu Mkuu nisaidie
    Kwa njia ya bank wanahitaji.
    Account Holder’s Name (The recipient’s full name)
    Account number (The recipient’s bank account number) *
    Bank Name (The name of the bank where the recipient’s account is heldBank Address (The address of the recipient’s bank),,,
    IBAN (The International Bank Account NumberSort Code (UK Bank codeRouting Number (ABA Routing Number)IFSC Code (Indian Financial System Code)
    Ndivyo hivi Mkuu na bank account sinabado. Nisaidie Sir.?

  7. Je kama na card yangu ya bank alafu nikajiunga na PayPal itawezekan na kam itakubal,endapo nitakuwa nalipwa mshahara hakutakuwa na wizi kwenye card yangu pale nitakapo toa namba za card naviambatanisho vyote…

  8. Vip sasa kama kunamtu anataka kutuma pesa yeye mfano kutoka Nigeria na Kenya kuja Tanzania inakuwa hii PayPal
    Naomba majibu tafathar

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use