in

Yote Yaliyojiri Kwenye Mkutano wa Google I/O wa Mwaka 2017

Ulipitwa na Mkutano wa Google I/O wa mwaka huu haya ndio yote yaliojiri

Hapo jana kampuni ya Google ilifanya mkutano wake mkubwa unafanyika kila mwaka unaoitwa Google I/O, mikutano hii hutumiwa na Google kuleta bidhaa mpya na kutangaza maboresho ya bidhaa zilizopo pamoja na mategemeo ya kampuni hiyo kwa miaka ijayo.

Hivi karibuni kwenye mkutano wa mwaka huu 2017 Google kama kawaida yake imetangaza bidhaa mpya pamoja na kufanya maboresho mengi zaidi kwenye bidhaa zake za sasa kama unataka kujua yote yaliyojiri kwenye mkutano huo endelea kuwa nasi.

  • Google Yatangaza “Lens”

Hapo jana kampuni ya google ilitangaza programu mpya iitwayo Lens, hii itakuwa na uwezo wa kutumia kamera ya simu yako kama kifaa cha kutambua nini kilichopo mbele yako, kwa mfano kama unataka kujua kuhusu mgahawa flani uliofika utakachofanya ni kuchukua simu yako na kuwa washa programu hiyo na kuelekeza kamera kwenye mgahawa huo na programu ya “Lens” itakupa maelezo kamili kuhusu mgahawa huo.

  • Google Yaleta “Smart Reply”

Kama umechoka kuandika email kila mara sasa programu ya Gmail ya Android na iOS sasa imeongezewa uwezo wa kujibu email yenyewe kwa kutumia sehemu mpya inayoitwa Smart Reply. sehemu hii itakusaidia kufupisha mda wa kuandika email kwa kukuletea uwezo wa kuchagua kujibu unachotaka kutoka kwenye machaguo ambayo yatakuja moja kwa moja kwenye programu hiyo.

  • Google Yaleta “Android Go”
Video: Kutana na Magari Mapya ya Kushangaza Mwaka (2020)

Kama sehemu ya mkutano wa Google I/O kampuni ya Google imetangaza toleo jipya la Android litakalo itwa Android Go, toleo hili litaweza kuwa msaada mkubwa kwa wale wenye simu zenye uwezo mdogo kama vile simu zenye RAM ya GB 1 au hata zile zenye uwezo wa RAM ya 512. Toleo hilo jipya litakuja kama sehemu ya Toleo jipya la “Android O” ambalo ndio toleo jipya kabisa la Android ambalo kwa sasa lipo kwenye majaribio.

  • Google Yaleta Huduma ya “VPS” (Visual Positioning Service)

Kwenye mkutano huo pia Google imeleta huduma mpya ya VPS au visual positioning service hii ni huduma ambayo itakuwezesha kutengeneza ramani ya ndani ya majengo mbalimbali yaani kama ilivyo Google Map lakini sasa hii itaonyesha ramani ya ndani ya majengo, kwa mfano kama umeingia supermarket na unataka majani ya chai unaweza kutumia huduma hiyo kuangalia kwenye ramani kujua mahali bidhaa hiyo inapo patikana ndani ya jengo la hilo la supermarket.

  • Google Yaleta Google Jobs
Sunday Movie #2 : Movie Nzuri ya Teknolojia ya Kuangalia

Google nayo imeamua kujikita kwenye swala zima la kuunganisha mtafuta ajira na mtoa ajira, yote hayo kupitia huduma yake mpya ya Google Jobs. Hapa watoa ajira na wanao tafuta ajira wote wataweza kujumuika moja kwa moja kwenye mtandao huo ili kuendeleza na kurahisisha swala zima la utafutaji na utoaji wa ajira kwani mtandao huo utaweza kukuonyesha kazi kutoka eneo ulilopo.

Na hayo ndio baadhi ya mambo mapya ambayo Google iliytangaza jana kwenye mkutano wake wa Google I/O, kusindikiza hayo pia Google ilitangaza baadhi ya maboresho ya programu zake za Youtube, Google Photos pamoja na kifaa cha Google Home, kama unaweza kuangalia video hapo juu kujua yote yalio jiri.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.