in

LG Yazindua Kioo Kikubwa cha Kompyuta cha Inch 42.5

Sasa LG inakuja na monitor hii kubwa yenye uwezo wa vioo vinne vya kompyuta

LG

Kampuni ya LG sasa imetangaza kuja na kioo kikubwa cha inch 42.5 kwaajili ya kompyuta, kioo hicho ambacho kinauwezo wa kuenea vioo vinne vya kawaida kinakuja na teknolojia ya UHD huku ikiwa na resolution ya 3840×2160 kwa maana nyingine kioo hichi kinauwezo wa teknolojia mpya ya 4K.

Mzigo huu kutoka LG unakuja na sehemu au port nne za kuchomeka waya (cable) za HDMI pamoja na sehemu mbili za kuchomeka USB zikiwa na uwezo wa USB 3.0 zote zikiwa zime tengenezwa kwa teknolojia ya  KVM switch, haija ishia hapo kuongezea kwenye kioo hicho sasa kuna sehemu ya USB Type-C yenye teknolojia ya DP Alt Mode pamoja na spika mbili za harmon/kardon speakers  zenye uwezo wa 10W huku ikiwa na sehemu ya headphone jack kwaajili ya kuchomeka spika au hadphone za nje.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kioo hicho chenye jina la 43UD79-B kinakuja pia na remote ambayo unaweza kutumia kwa matumizi mbalimbali kama vile kufanya full screen, kuzima na kuwasha, kuongeza mwanga, kuongeza sauti, kurekebisha aina ya picha na mengine mengi.

[envira-gallery id=”10591″]

Kioo hichi kinategemea kutoka mwezi May 19th, 2017 kwa nchini japan na inategemewa kuuzwa kwa dollar za kimarekani $745 USD sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,700,000. Itakubidi usubiri mpaka mwezi wa sita au wa saba mpaka kuipata hii kwa hapa Tanzania.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

LG Yazindua Kioo Kikubwa cha Kompyuta cha Inch 42.5
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.