Ripoti: iPhone 8 Inaweza Kuchelewa Kutoka Mwaka Huu

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Apple huenda iPhone 8 isitoke mpaka 2018
iphone 8 iphone 8

Wachambuzi kutoka Deutsche Bank wametoa ripoti kupitia mtandao wa ValueWalk kuwa, huenda simu mpya kutoka kampuni ya Apple iPhone 8 ikachelewa kutoka mwaka huu. Ripoti hiyo inaongeza kuwa kuchelewa kutoka kwa simu hiyo ni sababu ya kukosekana kwa baadi ya vifaa vya kutengeneza simu hiyo pamoja na changamoto za kiufundi.

Katika ripoti nyingine kutoka kampuni ya Foxconn inayo jihusisha na utengenezaji wa baadhi ya vifaa vya Apple imesema kuwa, iPhone 8 itachelewa kabisa mwaka huu na badala yake watumiaji wa simu hizo kutoka Apple watapata matoleo ya iPhone 7 pamoja na iPhone 7 plus yaliyo boreshwa zaidi. Hata hivyo katika ripoti zilizo tolewa wiki mbili zilizo pita zilikuwa zikibainisha kuwa uzalishaji wa simu hizo za iPhone 8 ungechelewa na kuanza mwezi October au November hivyo upatikanaji wa simu hizo sokoni ungekuwa ni mpaka mwaka 2018.

Bado kuna ripoti nyingi sana kutoka kwenye mitandao mbalimbali zikisema kuwa huenda simu hiyo isitoke kabisa mwaka huu, hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya theverge bado kampuni ya Apple hawaja zungumza lolote kuhusiana na hili hivyo itakubidi kusubiri taarifa kutoka kampuni ya Apple ili kupata uhakika zaidi kuhusu hili.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use