Wote tunafahamu kampuni ya Huawei kama kampuni maarufu ya utengenezaji wa simu, tablet pamoja na smartwatches lakini sasa ongeza kwenye list hiyo laptop, kwani hivi karibuni kampuni ya Huawei imezindua laptop yake ya kwanza inayoitwa Huawei Matebook X pamoja na Matebook D.
Inaweza kuwa hii ndio laptop ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Huawei lakini kwa muundo wake laptop hiyo ya Matebook X inafanana kabisa na laptop ya Macbook ya inch 12.
Tofauti iliyopo kubwa ni kwa baadhi ya sifa za laptop hii kwani laptop hii inakuja na uwezo wa Windows 10 pamoja na sifa zingine zifuatazo
- 2,160×1,440-pixel resolution screen (non-touch)
- Intel Core i5 or i7 CPU
- 8GB RAM
- 256GB/512GB SSD
- Full-size Chiclet backlit keyboard
- Two USB-C ports
- Includes multiport adapter
- Estimated 10-hour battery life
Picha nyingine za laptop hii hizi hapa
Kampuni ya Huawei Yajikita Rasmi Kwenye Biashara ya Laptop na Hii Ndio Laptop ya Kwanza Kutoka Kampuni Hiyo. https://t.co/nMZd3uJMP9 pic.twitter.com/uowdGd9pae
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) May 31, 2017
Kingine cha msingi ni kuwa laptop hii inakuja na rangi nne tofauti rangi hizo ni gold, grey pamoja pink na vilevile laptop hiyo inakuja kwa matoleo mawili tofauti ya Huawei Matebook X na Huawei Matebook D sifa za Matebook D ni kama zifuatazo.
- 15.6-inch 1,920×1,080-pixel resolution (non-touch)
- 7th gen Intel i5 or i7 CPU
- Estimated 8.5 hour battery life
- Dolby Atmos sound system
- Up to 1TB HDD
- Full USB, USB-C and HDMI ports
Sifa zingine za laptop hii unaweza kuangalia video hapo chini kujua kuhusu laptop hizi mpya kutoka kampuni maarufu ya huawei ambazo zinategemewa kuingia sokoni hivi karibuni.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.