Programu ya Siri Kuweza Kusoma Kwa Sauti Meseji za WhatsApp

Watumiaji wa iphone watafaidika zaidi na toleo jipya la programu ya WhatsApp
Siri Siri

Watumiaji wa simu za iphone sasa wanaweza kufaidika na toleo jipya la programu ya Whatsapp kwani sasa programu ya siri imewezeshwa kusoma meseji zako za whatsapp kwa sauti. Katika toleo hilo jipya la Whatsapp watumiaji wataweza kuwasha sehemu hiyo kupitia settings za programu ya Whatsapp.

Mtumiaji ataweza kuamuru siri kusoma meseji za whatsapp kwa kusema maneno ya “Hey Siri”, kumbuka ili kupata sehemu hii nilazima kuwasha shemu hiyo kupitia programu ya whatsapp kwa kwenda kwenye settings menu. Kwa kutumia sehemu hiyo mpya unaweza kujibu meseji pia kwa kusema kusema maneno na programu hiyo itakusaidia kuandika.

Kwa bahati mbaya kama wewe unatumia toleo la chini ya iOS 10.3 hutoweza kupata sehemu hiyo hivyo kama bado huja update simu yako ya iphone kwenda kwenye toleo jipya basi fanya hivyo kwa kudownload toleo jipya la iOS 10.3 sasa ili uweze ku-enjoy sehemu hiyo mpya.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use