Kampuni maaufu ya HTC hivi karibuni imetangaza tarehe halisi ya kuzindua simu yake mpya ya HTC OCEN ambayo itakuja na teknolojia mpya ambayo haijawahi kutumiaka wala kuonekana kwenye kampuni nyingine ya simu.
Teknolojia hiyo ambayo inaitwa Edge Sense inategemewa kuwepo kwenye simu hiyo ambayo itakupa uwezo wa kutumia pembe za simu yako kama vile touch screen, sehemu hiyo itakusaidia kutumia sehemu hiyo kufungua programu yoyote ambayo utakuwa ume set kwenye simu yako.
Kwa mujibu wa tovuti ya venturebeat simu hii inatarajiwa kutoka tarehe 16 ya mwezi may mwaka huu uku ikiwa na kioo cha inch 5.5 chanye resolution ya 2,560 x 1,440 pixel pamoja na kamera ya megapixel 12 ya mbele pamoja na kamera ya nyuma ya megapixel 16. kwa habari zaidi za simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.