in

Google Yaleta Auto Draw Programu Mpya Kwaajili ya Kuchora

Sasa ni rahisi kuchora kwa haraka na bila kuwa na ujuzi wowote

Kampuni maarufu kwa ubunifu wa teknolojia mbalimbali duniani Google hivi karibuni imezindua programu mpya inayoitwa Auto Draw, hii ni programu mpya ambayo itakuwezesha kuchora kwa haraka na kwa urahisi zaidi bila kuwa na ujuzi wowote wa kuchora.

Kwa kutumia teknolojia ya Sketch-RNN google imewezesha haya baada ya kufundisha mashine hiyo ya AI au (Artificial Intelligence) kuchora kupita michoro mbalimbali ambayo ilikua ikitumiaka kwenye programu ya majaribio ya Quick Draw iliyozinduliwa na Google hapo mwaka jana.

Kuhusu Auto Draw inavyofanya kazi programu hii ya mtandaoni itakuwezesha kuchora mchoro wako wa kawaida na yenyewe itaweza kugundua ni kitu gani unachora na kutoa mapendekezo kadhaa ya kitu unachotaka kuchora, programu hiyo pia itakupa uwezo wa kuweka rangi mbalimbali kwenye picha hiyo ikiwa pamoja na kuwezesha kuchukua picha hiyo ikiwa kwenye format ya png. Kumbuka kuwa programu hii haito chora kabisa unachotaka bali inakupa uwezo wa kuchagua aina ya mchoro unaotaka kuchora kutoka kwemye mapendekezo mbalimbali kulingana na mchoro ulio uchora.

Fahamu Njia Rahisi ya Kujua Mapato na Matumizi Yako

Programu hii itasaidia sana wale ambao wanataka kuchora michoro kwaajili ya vitu vidogo kama vile, watengenezaji wa programu mbalimbali za Android na iOS pamoja na watengenezaji wa tovuti kwani sasa itasaidia kurahisha katika utafutaji na utengenezaji wa ICON mbailmbali kwa urahisi zaidi. Unaweza kujaribu programu hiyo kwani ni nzuri kutumia bofya hapa kuijaribu.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.