Baada ya simu mpya ya Samsung Galaxy S8 kutoka wengi wameonekana kupendezwa na muundo pamoja na uwezo wa simu hiyo kwa ujumla lakini kilichopendeza zaidi kwenye simu hii ni uwezo wa kutumia simu hii kwenye kompyuta kwa kutumia kifaa kipya cha Samsung Dex.
Samsung Dex ni kifaa ambacho unaweza kuchomeka simu yako ya Galaxy S8 au Galaxy S8+ na simu hiyo itakuwezesha kutumia simu yako kwa kutumia keyboard na mouse kifupi ni kwamba utapata uwezo wa kutumia simu yako kama kompyuta huku ukiwa na uwezo wa kutumia programu za Microsoft Excel, Microsoft PowerPoint, Adobe Photoshop Lightroom pamoja na zingine nyingi.
Haija ishia hapo unapotumia kifaa hicho bado unakuwa na uwezo wa kutumia simu yako kama kawaida huku ukipata uwezo wa kujibu na kuandika meseji kwenye programu yoyote, zaidi ni kwamba kifaa hichi cha Samsung Dex kimewezeshwa na programu ambazo zinauwezo wa kusaidia kutumia kompyuta yako yenye mfumo wako wa Windows moja kwa moja kwenye kifaa chako. Kifaa hicho pia kimetengenezwa na feni ambayo inauwezo wa kupooza kifaa hicho pale kinapo tumiaka kwa sana.
Ili kutumia kifaa hicho unaweza kuchomeka kifaa hicho kwa kutumia waya za HDMI ambazo zinakupa uwezo wa 4K pamoja na sehemu ya Ethernet ambayo unaweza kutumia kuchomeka internet kwenye simu yako pamoja na mambo mengine pia kifaa hicho kinakuja na USB C port ambayo ni sehemu ya kuchaji kifaa chako. Kwa sasa kifaa hicho bado hakija tangazwa bei yake wala siku ya kutoka lakini pia kifaa hicho hakita uzwa pamoja na simu hiyo ya Samsung Galaxy S8. Endele kutembea Tanzania Tech tutakujulisha pindi kifaa hicho kitakapo toka.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.