in

Woolet Pochi ya Kisasa ya Kiume Isiyo Potea wala Kuibiwa

Umekua ukipoteza au kuibiwa wallet yako mara kwa mara..? soma hii

Wallet au pochi za kiume zimekua zikibadilika kadri miaka inavyokwenda, kumekuwa na wallet nyingi sana za bei ghali na hata zile za bei rahisi, lakini kwa sasa nataka nikwambie kidogo kuhusu wallet hii mpya ya Woolet.

Woolet ni wallet ya kisasa iliyo tengenezwa na kampuni moja inayochipukia ya Woolet yenye makazi yake huko california nchini marekani, kampuni hii imefanikiwa kuchanganya teknolojia na vitu vya asili ili kuwezesha kukuletea pochi hii ya kisasa ambayo hutoweza kuipoteza au kuibiwa kirahisi.

Wallet hii imetengenezwa na ngozi halisi pamoja na teknolojia nyingine ambazo zinafanya uweze kupata taarifa kwenye simu yako ya mkononi pale unapo-ibiwa, kusahau au kupoteza wallet au pochi yako.

Pochi hii inakupa uwezo mkubwa wa kupokea ujumbe mfupi SMS pamoja na sauti ambayo itaweza kukujulisha kwamba pochi yako au wallet yako imesaulika, zaidi wallet hii inakupa uwezo wa kuweza kujua mahali ilipo pale unapo isahau au kuipoteza kwenye mazingira flani. Woolet kwa kupitia App yake utaweza kuweka kiasi cha umbali kutoka kwenye simu yako na wallet yako, umbali huo ndio utakaokupa uwezo wa kupata ujumbe pale unapo sahau pochi au wallet yako, woolet inaendeshwa na sensor maalum pamoja na battery yenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi ya miezi mitano.

Hatimaye Apple Yaleta Huduma ya Apple Music Nchini Tanzania

Woolet inapatikana kwa size mbalimbali pamoja na rangi tofauti, pochi hizo za woolet zinauzwa kwa bei tofauti kutokana na sifa zake unaweza ukangalia bei zake kupitia tovuti ya Woolet hapa unaweza pia kupata taarifa zaidi kuhusu wallet hiyo kupitia tovuti hiyo.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech au download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia jiunge nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 3

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.