in

Vodacom Tanzania Yazindua App Mpya ya Android ya M-Pesa

Sasa fanya miamala yako ya pesa kwa njia mpya, haraka na bora zaidi ya M-Pesa App

m-pesa

Kampuni na mtandao wa simu maarufu wa Vodacom Tanzania leo umeingia hatua nyingine baada ya kuzindua programu yake ya M-Pesa kwaajili ya kufanya miamala yako kwa urahisi zaidi, App hiyo ambayo imetoka kwa mfumo wa Android itakuwezesha kutuma pesa kwa njia ya kisasa zaidi huku ikikupa uwezo mkubwa wa kuendesha akaunti yako kuliko hapo awali.

Programu hiyo inakupa uwezo wa kutuma pesa kwa haraka uku ukiweza kuchagua viwango vya fedha bila kuandika kila mara utakapo taka kutuma pesa vilevile programu hiyo inakupa uwezo wa kutuma pesa kwenda kwenye mitandao yote ikiwemo mtandao wa Safaricom wa nchini Kenya. Programu hii ya M-Pesa kwa sasa itakupa uwezo wa kutuma pesa moja kwa moja kutoka kwenye phonebook yako kwa kurahisisha kuchagua namba ya mtu kwa haraka zaidi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kifupi ni kwamba programu hii mpya ya M-Pesa ina mabadiliko makubwa sana na uwezo mzuri sana wa kukusaidia kufanya miamala yako kwa urahisi na kwa ulinzi zaidi, kama unataka kujionea mwenyewe unaweza kudownload App hiyo kupitia Play Store au unaweza kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye ukurasa maalumu ili kudownload programu hiyo.

M-Pesa Tanzania
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Vodacom Tanzania Yazindua App Mpya ya Android ya M-Pesa
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment