Ni takriban miezi sita au saba imepita toka kampuni ya Sony kuzindua mfululizo wa simu zake za Sony Xperia XZ. Mwaka huu kampuni hiyo imeamua kuongeza mfululizo wa matoleo hayo kwa kuleta simu mpya za Xperia XZ Premium pamoja na Xperia XZS zote za mwaka 2017.
Kwa wapenzi wa simu za Sony simu hizi hasa Xperia XZS inafanana sana na simu ya mwaka jana ya Sony Xperia XZ, ambayo ilitoka rasmi mwezi october mwaka 2016. XZ Premium yenyewe inaonyesha mabadiliko makubwa kuanzia kava lake la nje ambalo sasa ni la chuma mpaka sifa za ndani ambazo sasa zimeboreshwa zaidi tofauti na Xperia XZS.
Sony Xperia XZ Premium imeongezewa vitu kama Qualcomm Snapdragon 835 processor, 4GB RAM pia imepunguzwa mpaka mm 7.9 pia simu hiyo sasa imewekewa teknolojia ya kuzia maji ya IP68 waterproofing ambayo inaweza kuimili mpaka maji metres 1.5 (5 feet) kwa dakika 30, pia battery nayo imeongezwa na kuwa 2,900mAh pamoja na kamera ya mbele ambayo sasa imekuwa megapixel 13, kwa upande wa mfumo wa uendeshaji simu hiyo sasa inatumia Android 7 Nougat huku ikiwa na ukubwa wa GB 64 za ukubwa wa ndani ambao unaweza kuongezeka kwa memory kadi ya mpaka GB 256.
Kwa upande wa Sony Xperia XZS ya mwaka huu 2017 kama nilivyo sema hapo awali simu hii haina kilicho ongezewa sana bali sasa simu hiyo ina kioo kikubwa cha inch-5.2 pamoja na ukubwa wa battery wa 2,900mAh ikiwa nayo imewezeshwa kutumia mfumo mpya wa uendeshaji wa Android 7.0 Nougat vitu vingine vyote vilivyo baki bado viko kama kwenye toleo la simu hiyo ya mwaka jana yani 2016.
Kuhusu Bei bado haijajulikana simu hizo zitauzwa kwa bei gani ila habari zinasema kuwa simu hizi zinategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi wa tatu mwishoni au wanne. Kama ulikua ujui sifa za simu hizi za mwaka 2016 bofya hapa kujua sifa hizo na hapa kujua sifa za Xperia XZ.