in

Muonekano wa Simu Mpya ya Samsung Galaxy S8 na S8+

Yajua yote ya muhimu kuhusu simu mpya ya Samsung Galaxy S8

Kwa wapenzi wa simu za Samsung Galaxy leo kampuni ya Samsung Mobile kwa mara nyingne tena imezindua simu yake bomba ya Samsung Galaxy S8, wakati nikiwa na shauku ya kukwambia yote ya muhimu kuhusu Samsung Galaxy S8 basi kama ulipitwa na tamasha la uzinduzi wa simu hii usijali kwani unaweza kuangalia tukio lote kupitia hapa Tanzania Tech.

Samsung Galaxy S8 imetengenezwa kwa muundo wa tofauti kabisa simu hii imetengenezwa kwa muundo mpya ambao unakupa uwezo wa kutumia simu yako zaidi kuliko hapo awali. Samsung pia imebadilisha namna nzima ambayo ulikua umezoea kutumia simu yako, kifupi ni kwamba simu hii imekua ya tofauti kabisa kuliko simu zingine zote ambazo zimewahi kutengenezwa na Kampuni ya Samsung. Hapa ni malizie kwa kukwambia kuwa simu hii imebadili sana kuanzia muundo mzima mpaka uwezo wake halisi.

Muundo wa Samsung Galaxy S8 bado ni kitu cha kuzungumzia kwani muundo huu mpya wa bezels unafanya simu ya Galaxy S8 kuwa yenye kioo kitupu kwa asilimia 95. Huku ikikupa uwezo wa kutumia simu yako kwenye kioo kikubwa zaidi. Pia Galaxy S8 inakuja bila kuwepo na kibonyezo cha home, bali sasa simu hiyo itakuja na kibonyezo cha home kisicho onekana hivyo utabofya kwenye kioo cha simu yako ili kurudi mwanzo au Home.

Jiandae na Infinix S5 Pro Hapa Tanzania (10 April 2020)

Vilevile Unapo nunua simu hii ya Galaxy S8 inakuja na vifaa mbalimbali ndani ya box lake vifaa hivyo ni kama vile Handset, Earphones za tuned by AKG, Waya wa USB Type-C Cable, Chaji ya Kusafiria, USB Connector (C to A), Micro USB Connector (C to B), Ejection Pin pamoja na Ear Tips vyote vikiwa ndani ya Box lako.

Ukweli ni kwamba yako mengi sana ya kuzungumzia kuhusu simu hii mpya na kama unataka kuyajua yote endelea kutembelea Tanzania Tech kwani tutakuleta sifa kamili za simu hii ya Samsung Galaxy S8, kwa sasa kwa mhutasari hizi ndio sifa chache za Samsung Galaxy S8

SifaGalaxy S8Galaxy S8+
Kioo5.8 inches6.2 inches
Ukubwa148.9 x 68.1 x 8mm, 155g159.5 x 73.4 x 8.1mm, 173g
Kamera12MP main, 8MP front12MP main, 8MP front
Memory Ndani64GB + MicroSD64GB + MicroSD
Mfumo OSAndroid 7.0Android 7.0
Siku ya KutokaApril 28  (April 20 kuagiza)April 28  (April 20 kuagiza)
BeiTsh 1,700,000Tsh 2,000,000
Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy M31

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.