Microsoft Yashitakiwa Baada ya Kutoa Toleo Jipya la Windows 10

Kuwa mwangalifu kila unapotaka ku-update kompyuta yako kwenda kwenye toleo jipya
Windows 10 Windows 10
PICHA NA TECHRADAR

Nchini marekani kampuni ya Microsoft ambayo ndio inayo tengeneza programu ya Windows 10 inakabiliwa na mashtaka baada ya watumiaji kadhaa kulalamika kuwa, mara baada ya ku-update kompyuta zao kwenda kwenye toleo jipya la programu hiyo ya Windows 10 kompyuta zao zilizima na nyingine kupoteza baadhi ya data muhimu kutoka kwenye kompyuta zao.

Kwa mujibu wa tovuti ya techradar.com tatizo hili linatokea kwa watumiaji nchini humo wanao update kompyuta zao kutoka matoleo ya Windows 7 pamoja na Windows 8.1 kwenda kwenye toleo hilo jipya la Windows 10. Katika ripoti nyingine iliyotolewa na tovuti ya theregister.co.uk inasema kuwa mashtaka hayo yamefunguliwa na watu watatu huko Illinois na sasa mashtaka hayo yanategemewa kujumuisha watu wote ambao wamepata matatizo kama hayo huko nchini marekani.

Katika moja ya mashtaka hayo Stephanie Watson, alikuta kompyuta yake imefanya update za Windows 10 na kufuta baadhi ya vitu ambavyo vingine vilikua muhimu kwenye kazi yake, pamoja na Stephanie kuleta mtaalamu wa kurudisha baadhi ya data hizo lakini zoezi hilo halikufanikiwa kwa asilimia 100 na matokeo yake mtumiaji huyo aliamua kununua kompyuta nyingine.

Advertisement

Hata hivyo kwa mujibu wa wakili anae wakilisha watu hao anaema kuwa, kuna watu zaidi nchini humo ambao wamepata matatizo ya kuharibika kwa kompyuta zao au kupoteza data kutokana na ku-update kompyuta zao kwenda kwenye Toleo jipya la Windows 10. Microsoft imenukuliwa ikitoa majibu kuwa, mashtaka hayo ni yakijinga kwani programu hiyo inayo sehemu ya kurudisha toleo la zamani ndani ya siku 31 yaani mwezi mzima.

Hata hivyo inajulikana kuwa sehemu hiyo inayo tabia ya kukata kufanya kazi na kushindwa kurudisha vitu vyote pale mtu unapotaka kufanya hivyo kama vile kwenye tukio lililo tokea kwa mmoja wa walala mikaji wa sakata hili. Inashauriwa kufanya backup ya vitu vyako vya muhimu kabla ya kufanya update zozote za Windows 10 na matoleo mengine.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use