in

Jinsi ya Kupiga na Kupokea Simu kwa Kutumia Kompyuta Yako

Jifunze hapa jinsi ya kupiga na kupokea simu kwenye kompyuta

kupiga simu kwenye kompyuta

Wote tunajua kuna wakati unajikuta huwezi kutumia simu yako labda kutokana na muda mwingi unajikuta unafanya kazi kwenye kompyuta hivyo inakuwia vigumu kushika simu yako kila saa, kukusaidia katika hilo leo Tanzania Tech tunakuletea njia hii rahisi ya kuwezesha kupiga na kupokea simu yako kwa kutumia kompyuta yako.

Basi kwa kuanza hatua hizi unatakiwa kuwa na baadhi ya vitu vifuatavyo, unatakiwa kuwa na kompyuta ambayo ina uwezo wa kutumia wifi pia unatakiwa kuwa na simu ya android yenye uwezo wa kutumia wifi. Baada ya kuhakikisha una vitu vyote hivi basi unaweza kuendelea kwa kufuata hatua hizi rahisi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hatua ya kwanza hakikisha una internet ya kutosha kuweza kupakua programu hii kutoka Play Store, programu hii inaitwa Remote Phone Call Trial unaweza kudownload kwa ku-bofya hapo chini.

Kumbuka programu hii unaweza kutumia bure kwa muda wa siku 15 tu, kama utapenda kutumia zaidi programu hii inakubidi ununue programu hii ya kulipia na unaweza kutumia programu hii kwa muda wote utakao hitaji wewe. Baada ya kudownload programu hiyo kwenye simu yako basi ingia kwenye kompyuta yako kisha bofya hapa kudownload programu kwaajili ya kompyuta kisha install kwenye kompyuta yako na endelea kufuata hatua zingine.

Baada ya kudownload programu zote, washa programu zote za kwenye kompyuta pamoja na ile iliyoko kwenye simu yako kisha baada ya kuwasha programu zako utaona device IP na password hizo ziandike pembeni kwani utazingiza kwenye programu ya kwenye simu ambayo uliwasha awali, bofya sehemu ya add WiFi device kwenye programu hiyo ya simu alafu ingiza namba za device IP ambazo ulizi andika pembeni hapo awali, baada ya kuingiza device IP bofya ok kisha weka password kisha malizia kwa kuweka namba unazoziona kwenye kioo cha kompyuta yako baada ya kumaliza hatua zote hizo utakuwa umemaliza na uko tayari kutumia simu yako kwenye kompyuta.

Kwa mafunzo zaidi ya teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku au unaweza ku-download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store, pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel ya Tanzania tech kupitia youtube ili kujifunza maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Jinsi ya Kupiga na Kupokea Simu kwa Kutumia Kompyuta Yako
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

20 Comments

  1. Hongereni sana kwa kazi nzuri ya kuelimisha watumiaji wa Laptop na Sim,kiukweli mmekua msaada mkubwa sana kwa sisi wadau na wapenzi wa vitu hivi.kikubwa msikate tamaa kwani kila kazi inachangamoto zake.kazi njema.

  2. Kwani Tanzania Tech nimewapenda hata mlipoanza hii website yenu nilikuona kama masihara hivi mi kila hatua unayoenda nakufuatilia uko viziri ndugu.Safi sana!
    KWanini website yako usiiweke watu watembelee bure kwenye app ya FreeBasics?