Headphone Zalipuka Kwenye Ndege na Kumjerui Mwanamke

Sakata jipya la headphone kulipuka kwenye ndege ya kwenda nchini Australia
Headphone zalipuka Headphone zalipuka

Mwanamke mmoja aliyekua anasafiri na ndege kuelekea nchi ya Australia ambae jina lake alikujulikana kwa mara moja, amejeruhiwa usoni kwa mlipuko wa battery iliyokuwa kwenye headphone alizokua anasikiliza muziki akiwa kwenye ndege hiyo.

Mwanamke huyo alisema kuwa alishtuka na kuziondoa headphone hizo kutoka masikioni kwa haraka kitendo kilichosababisha headphone hizo kuangukia shingoni uku zikiendelea kutoa moshi na moto kidogo. Mwanamke huyo anaendelea kusema alizitoa headphone hizo shingoni na kuziangusha kwenye sakafu ya ndege ambapo muhudumu wa ndege aliweza kusaidia kwa kumwagia maji headphone hizo ambazo tayari zilikua zimesha mjerui mwanamke huyo.

Hata hivyo mamlaka inayoshulikia usalama wa usafirishaji ya nchini Australia Australian Transport Safety Bureau (ATSB) haikuweka wazi jina la mwanamke huyo wala jina la ndege iliyohusika pamoja na jina la headphone hizo ambazo zimemjerui mwanamke huyo.

Advertisement

Mamlaka hiyo kwa sasa bado inafanya uchunguzi huku ikiwataka wasafiri kuwa makini na battery zote za lithum pamoja na kutaka vifaa vyote vinavyotumia battery vichunguzwe kabla ya kuruhusiwa kuingia ndani ya ndege. Hata hivyo vifaa vinavyo tumia battery kwa sasa vina endelea kuongezeka kwa kasi huku usalama wa watu ukiwa wa kusua sua, mwaka jana mamlaka ya usalama ya usafirishaji ya marekani ilipiga marufuku utumiaji wa simu za Samsung Galaxy Note 7 baada ya simu hiyo kulipuka kwenye ndege na kusababisha wasafiri kuwa na wasiwasi lakini hakuna mtu yoyote aliye jeruhiwa kwenye tukio hilo lililo chukua vichwa vya habari kwenye mitandao mbalimbali hapo mwaka jana.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku au unaweza kupata habari kwa haraka kwa kudownload App ya Tanzania Tech, pia usisahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use