Facebook Yaleta Messenger Day Sehemu Nyingine Kutoka Snapchat

Facebook inaendelea kuchukua sehemu za mtandao wa snapchat bila wasiwasi
Messenger Day Messenger Day

Hivi karibuni mtandao wa facebook umeleta sehemu mpya iitwayo Messenger Day, sehemu hii kama zilivyo baadhi ya sehemu mpya za mitandao ya instagram na facebook ni moja kati ya sehemu zilizo anzia kwenye mtandao wa kijamii ya Snapchat.

Sehemu hiyo kama ilivyokuwa kwenye programu ya Snapchat mtumiaji atapewa nafasi ya kuweka picha na video kupitia programu ya Facebook messenger na picha hizo au video zitapotea baada ya masaa 24. Sehemu hiyo mpya itakuruhusu kuweka urembo mbalimbali kwenye picha hizo kama vile maandishi yenye rangi mbalimbali, sticker na urembo mwingine unao patikana kwenye programu hiyo ya Facebook Messenger.

https://www.facebook.com/messenger/videos/1227636360689375/

Advertisement

Habari zinasema sehemu hii mpya ilianza kujaribiwa toka mwezi September, 2016 huko nchini Poland na sasa iko tayari kutoka kwa dunia nzima baada ya majaribio hayo ambayo yanaonekana yalienda vizuri. Sehemu hiyo kwa sasa inapatikana kwenye Facebook Messenger na kama bado hujaipati hakikisha una update programu yako ya Facebook Messenger ili kupata sehemu hiyo mpya.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech au unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use