Eye Kava lenye Uwezo wa Mfumo wa Android kwenye iPhone

Tumia Android kwenye simu yako ya iPhone
Kava la Eye Kava la Eye

Teknolojia inaendelea kukua kila siku hata yale ambayo tulikua tuna hisi hayawezekani kwa sasa yanawezekana, kampuni nyingi sana kwa sasa zimejikita kwenye utengenezaji wa simu ambazo ni 2 in 1 yaani simu zenye uwezo wa kutumia mfumo wa Android na iOS kwa pamoja.

Hapa Tanzania tech tumesha ona kava la simu lenye uwezo wa kubadilisha simu ya iphone kuwa android lakini sasa leo nakuletea hii ya kava lenye uwezo wa kuweka mfumo wa Android na iOS kwenye simu moja. Kava hili lenye jina la Eye lina uwezo wa kuongeza kioo kingine kwa upande wa pili ili kukupa uwezo wa kutumia Android kwenye simu yako ya iphone.

Advertisement

Kava hilo la Eye linatumia kamera, kinasa sauti (mic) pamoja na speaker za simu ya iphone lakini pia kava hilo lina sehemu ya kuweka line ya simu pamoja na sehemu ya kuweka memory card ambavyo vyote vina jitegemea. Vilevile kava hilo linatumia battery yake yenyewe ambayo inafanya kioo hicho kuwa na chaji yenye kudumu karibia masaa 24, kava hilo ambalo ni simu ya Android liko kama vile umegundisha simu ya android kwa nyuma ya simu ya iphone.

Kava la Eye linauzwa kwa dollar za marekani $95 sawa na shilingi za tanzania Tsh 220,000 kwa kava lisilo na 4G na dollar za marekani $129 sawa na shilingi za tanzania 290,000 kwa kava la lenye uwezo wa 4G. Kwa habari zaidi kuhusu kava hili unaweza kutembelea tovuti ya ESTI Inc.

Kama unataka habari zaidi za teknolojia pamoja na mafunzo mbalimbali ya teknolojia usiache kujiunga nasi kupitia App ya Tanzania Tech pamoja na Channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use