WhatsApp Yatoa Two Step Verification kwa Watumiaji Wote

Sehemu hii ni ya muhimu sana kuiwasha sasa
Two Step Verification Two Step Verification

Baada ya majaribio ya muda mrefu sasa WhatsApp iko tayari kuleta sehemu mpya ya Two Step Verification, sehemu hiyo ambayo iliyokua ikifanyiwa majaribio kwenye programu ya WhatsApp Beta sasa imekuja kwa watumiaji wote wa programu hiyo.

Sehemu hiyo kwa sasa ni sehemu ya muhimu sana kutokana na kuongeza ulinzi imara kwenye programu hiyo, jinsi ya kuwasha sehemu hiyo utaingia kwenye programu ya WhatsApp kisha ingia kwenye Account Settings kisha utaona sehemu hiyo mpya ambapo utatakiwa kutengeneza password yenye tarakim nne ambazo utazitumia kila utakapo taka kusajili programu hiyo kwenye kifaa kingine.

WhatsApp imeleta njia hii wakati muafaka kwani itazuia watu ku-hack akaunti za watu wengine kwani kila unapotaka kuwasha programu hiyo kwenye simu nyingine utauliza namba hiyo ambayo kama umeisahau utaipata kwa njia ya email yako. Harakisha sasa update programu yako ya WhatsApp kisha ingia kwenye settings na angalia kama sehemu hiyo ya Two Step Verification imekuja na kama imekuja hakikisha unaiwasha haraka kuongeza ulinzi kwenye programu yako ya WhatsApp.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia download sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store au unaweza kujiunga na channel yetu ya Youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya Video.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use