Ufaransa Kutumia Ndege Aina ya Tai Kuangusha Drone za Magaidi

Ufaransa imeamua kuchukua hatua ya kujilinda kwa kutumia ndege aina ya tai
drones drones

Kadri teknolojia inavyozidi kukua ndivyo navyo baadhi ya watu wavyotumia teknolojia hiyo hiyo kufanya ugaidi na kuangamiza watu pamoja na makazi yao, ili kuhakikisha kuwa haya hayaendelei kutokea ufaransa imechukua hatua ya aina yake ya kujilinda na ndege zisizokua na abiria (Drone) kwa kufundisha ndege aina ya tai (eagles) kuangusha ndege hizo kutoka angani.

Ufaransa kwa sasa inamalizia kufundisha ndege hao na siku za karibuni ndege hao watapelekwa kwenye vilima vya pyrenees huko nchini ufaransa kwaajili ya majaribio ya mwisho. Kwa mujibu wa tovuti ya The Washington Post kamanda wa jeshi anae simamia mafunzo hayo alisema kuwa ndege hao wana-fundishwa wakiwa toka wadogo huku wakipewa zawadi ya nyama inayo fungwa nyuma ya ndege hizo pale wanapo fanikiwa kuziangusha.

Advertisement

Ufaransa imeamua kujilinda kwa kutumia ndege hao baada ya shambulizi la ugaidi lilotokea mwaka 2015 baada ya watu 130 kupoteza maisha na wengine zaidi ya miamoja kujeruhiwa kutokana na shambulio hilo lililo tokea kwenye baadhi ya miji nchini ufaransa.

Kwa habari zaidi za teknolojia usiache kutembelea Tanzania Tech kila siku pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kutoka Play Store ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi, pia kama unataka habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use