Baada ya kutoka kwa Huawei P9 sasa tumesha anza kusikia tetesi kuhusu simu mpya ya Huawei P10, simu hii inayotarajiwa kutoka mwanzoni mwa mwaka huu ni moja kati ya simu zinazotarajiwa kuwa na ubora wa hali ya juu pamoja na maboresho mengi.
Kwa sababu kazi yetu ni kukuletea habari zote za teknolojia basi ni vizuri kukupa habari kuhusu tetesi hizi za picha zilizosambaa mtandaoni siku za karibuni. Picha hizo zinaonekana kuonyesha simu inayothaniwa kuwa ni (renders) mfano wa simu za Huawei P10 pamoja na P10 Plus zikiwa na rangi ya nyeupe yenye gold (white-golden).
Simu hizi za Huawei P10 na P10 Plus zinategemewa kutuka kwenye mkutano wa CES wa mwaka huu 2017. Simu hizo pia zinategemewa kuja na sifa za simu hii inategemewa kuja na kioo cha inch 5.5, Ultrasonic fingerprint sensor, kamera mbili za nyuma zilizotengenezwa kwa teknolojia ya leica vyote vikiwa vinaendeshwa na processor ya Kirin 960 chip pamoja na Ram ya GB 4 ikiwezesha simu hizo kuifadhi data kwenye memory yake ya ndani ya GB 64 kwa Huawei P10 pamoja na GB 124 kwa Huawei P10 Plus.
Kuhusu tarehe ya kutangazwa kwa simu hii ya Huawei P10 inatarajiwa kutoka tarehe 26 February kwenye mkutano wa Mobile World Congress utakao fanyika uko nchini Barcelona.
Kama unataka kufuatilia habari mbalimbali kutoka hapa Tanzania Tech basi unaweza kufanya hivyo kwa kupakua App ya Tanzania Tech na utapokea habari zote za teknolojia pindi zitakapo toka. Pia unaweza kuungana nasi kupitia channel yetu ya youtube ili kujifunza mambo mbalimbali ya Teknolojia kwa njia ya video.
Inatoka lini hii simu
Mary Hii inatatoka mwaka huu endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.
Nimependa sana tovuti yenu
Asante sana Amina endelea kutemblea Tanzania Tech