Tetesi Nokia 3310 Kurudi Tena Kupitia Mkutano wa MWC

Kuna uwezekano wa ujio mpya wa Nokia 3310
Simu Nokia 3310 Simu Nokia 3310

Nokia 3310 ni moja kati ya simu ambazo ni simu baba kwenye ulimwengu mzima wa simu za mkononi, hivyo basi kama ulikua umeikosa simu hii jiandae kuiona tena mwaka huu tena ikiwezekana kabla ya mwisho wa mwezi huu february.

Kwa mujibu wa tovuti ya theverge pamoja na thenextweb  Nokia 3310 inatarajiwa kuja kupitia mkutano mkubwa wa Mobile World Congress utakao fanyika huko nchini Barcelona kuanzia tarehe 27 february mpaka March 2. Hata hivyo kwa mujibu wa makala kutoka kwenye tovuti hizo tetesi hizo zilitoka kwa Evan Blass mmoja kati ya watu wanaotegemewa sana kwenye ulimwengu mzima wa taarifa kuhusu ujio wa simu mpya.

Nokia inategemewa kutoa simu nyingine zenye kutumia Android kama Nokia 5  pamoja na Nokia 3 ambazo zinakadiriwa kuuzwa kwa €199 ( $210.87) pamoja na €149 ($157.89) sawa na makadirio ya shilingi za kitanzania Tsh 500,000 na Tsh 360,000.  Kwa upande wa Nokia 3310 simu hiyo iliyoboreshwa inategemewa kuuzwa kwa €59 ($62.61) sawa na makadirio ya shilingi za kitanzania Tsh 150,000.

Advertisement

Kwa taarifa kamili kuhusu tetesi hizi endelea kutembelea tanzania tech kila siku au unaweza kupakua App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa wakati, pia unaweza kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia youtube kama unataka kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use